Anaitwa Yuri Alexeyevich Gagarin alizaliwa tarehe 9 Machi 1934 huko Klushino karibu na Smolensk, Urusi; alifariki tarehe 27 Machi 1968. Alikuwa mwanaanga wa kwanza katika historia yaani mtu wa kwanza aliyefika kwenye 'Anga la nje' #Duniayako




Alimwoa Valentina Goryachova akawa na mabinti wawili ambao ni Galina na Yelena. Akajiunga na Jeshi la Anga ya Urusi mwaka 1955.



Mwaka 1960 aliteuliwa katika kikosi cha kwanza cha marubani walioandaliwa kurushwa kwa anga la nje akateuliwa kuwa mtu wa kwanza wa kutoka duniani.

Tarehe 12 Aprili 1961 alirushwa na chombo cha angani Vostok 1 akizunguka dunia lote mara moja katika muda wa dakika 108. Akashuka Siberia.

Alipandishwa cheo na kuwa mkuu wa kituo cha kuandaa wanaanga Warusi. Mwaka 1968  alikufa katika ajali ya ndege alipofanya mazoezi ya urubani akazikwa kwenye makaburi ya heshima huko Moscow.

Comments