Bilionea wa Denmark na mmiliki wa Kampuni ya ASOS, Anders Holch Povlsen ni miongoni mwa watu waliokubwa na balaa la kusikitisha baada ya kupoteza watoto wake watatu kati ya wanne nchini Sri Lanka kufuatia mashambulio mfululizo yaliyotokea jana, Jumapili siku ya pasaka na kuua watu takribani 290.
Msemaji wa bilionea huyo Povlsen, ambaye pia anamiliki eneo kubwa la makazi huko nchini Scotland, amethibitisha kutokea kwa vifo vya watoto hao bila kusema kuhusu wa nne.
Bilionea huyo alikuwa nchini humo kwaajili ya mapumziko ya sikukuu na familia yake lakini yeye na mkewe na mtoto wao mmoja wamepona.
Siku moja kabla ya shambulio hilo la kutisha, mmoja wa mtoto wa tajiri huyo, Alma alitupia picha katika ukurasa wake wa Instagram akiwaonesha ndugu zake Astrid, Agnes na Alfred, wakiwa jirani na bwawa la kuogelea.
Tajiri huyo mapema mwaka huu aliweka wazi mpango wake wa kuwaachia watoto wake umiliki wa utajiri wake wa makazi ili waweza kuendeleza malengo yake ya miaka 200 ijayo baada ya yeye kufa.
Sri Lankan imekilaumu kikundi kidogo cha Kiislamu cha ndani maarufu kama Thowheed Jamaath (NTJ) kuhusika na shambulio hilo la kigaidi na kuongeza kuwa walipata usaidizi kutoka kwa kundi la kimataifa', huku wakilitilia mashaka zaidi kundi la ISIS kuhusika.
Comments
Post a Comment