CAG AGOMA RASMI KUJIUZURU ADAI HAKUNA KIPENGERE KWENYE KATIBA ALICHOVUNGA KINACHOMLAZIMU AJIUZUKU

CAG AGOMA RASMI KUJIUZULU ADAI HAKUNA KIPENGELE KWENYE KATIBA ALICHOVUNJA KINACHOMLAZIMU AJIUZULU

MKAGUZI na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad, amegoma kujiuzulu kutoka kwenye wadhifa wake. Anaripoti Saed Kubenea … (endelea).
Taarifa kutoka kwa watu waliokaribu na kiongozi huyo, wakiwamo baadhi ya watendaji serikalini na katika Chama Cha Mapinduzi (CCM), zinaeleza kuwa juhudi za kumtaka Prof. Assad kujiuzulu, “zimegonga mwamba.”
“Amegoma kata kata kujuzulu. Amesema, ‘kinachoitwa mgogoro kati yake na Bunge,’ ni kitu kinachotengenezwa na watu wasiopenda kazi yake,” ameeleza ofisa mmoja mwandamizi serikalini ambaye jina lake tunalihifadhi.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, watu kadhaa walimfuata Prof. Assad ili kumshawishi kujiuzulu, lakini msimamo wa kiongozi huyo, ni kuwa suala la mgogoro wake na Bunge, siyo sehemu ya mambo ambayo yanamtaka kuachia ngazi.
Amesema, “siwezi kujiuzulu na kuondoka ofisini. Soma katiba, utaona sababu zinazoweza kumuondoa CAG madarakani. Hili la Bunge, siyo miongoni mwao,” anaeleza mtoa taarifa akimnukuu Prof. Assad.
Bunge la Tanzania la Jamhuri ya Muungano, lilipitisha azimio la kutokufanya kazi na CAG baada ya kumtuhumu kudharau chombo hicho na baadaye kumtia hatiani.
Prof. Assad alitiwa hatiani na Bunge baada ya kumtuhumu kulidhalilisha kufuatia kauli yake aliyoitoa katika mahojiano yake nad Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya Umoja wa Mataifa (UN), jijini New York nchini Marekani, Desemba mwaka 2018.
Katika mahojiano hayo na kituo hicho cha radio ya umoja wa mataifa, Prof. Assad alisema, Bunge la Tanzania halina meno na hivyo limeshindwa kuiwajibisha ipasavyo serikali.

Akifafanua kuhusu anachokiita, mgogoro huo kugeuka, suala la kikatiba,” Prof. Assad anasema, “tafsiri ya kuwa Bunge haliwezi kufanya kazi na CAG, ni tafsiri pana sana na inatakiwa tuijue vizuri.
Alipoulizwa iwapo aweza kujiuzulu, msomi huyo anayeheshimika nchini, haraka alisema, “nitataendelea kutekeleza majukumu yangu kama ilivyoainishwa kwenye katiba.”
Aidha, Prof. Assad aliwahi kuliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), kwamba “sina maamuzi ya kufanya zaidi ya kuomba dua watu waongoze vizuri na wafanye maamuzi yenye faida na nchi hii. Hilo ndilo ninaloweza kulifanya kwa sasa.”
Alikuwa akijibu swali la mtangazaji wa kituo hicho aliyetaka kujua kama anaweza kuchukua “maamuzi magumu ya kuachia ngazi.
Alisema, “…kama tunatoa ripoti na inaonekana kuna ubadhilifu, halafu hatua hazichukuliwi, huo kwangu mimi ni udhaifu. Bunge linatakiwa liisimamie serikali na kuhakikisha kuwa pahali penye matatizo basi hatua zinachukuliwa.
“Sisi kazi yetu ni kutoa ripoti tu; na huo udhaifu nafikiri ni jambo la kusikitisha, lakini ni jambo tunaamini muda si mrefu huenda likarekebishika.
“Tunadhani tatizo kubwa linatokana na Bunge kushindwa kufanya kazi yake kama linavyotakiwa,” alieleza Prof. Assad katika mahojiano yake na Radio ya UN.
Mara baada ya Ndugai kuongoza Bunge na kupitisha azimio hilo, wananchi waliowengi wameonekana kumuunga mkono Prof. Assad na wengine kufika mbali zaidi kwa kumtaka Spika kuachia ngazi.
Kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, CAG huondoka madarakani baada ya kufikisha umri wa kustaafu ama kujiuzulu wadhifa wake.
Ibara 144 ya katiba inaeleza kuwa CAG anaweza kuondolewa katika madaraka ya kazi yake kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi zake (ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote) au kwa sababu ya tabia mbaya, au kwa kuvunja masharti ya sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Hata hivyo, kuna utaratibu maalumu wa kumwondoa ambapo Ibara ya 144 (3) inabainisha kuwa iwapo rais ataona kwamba suala la kumwondoa kazini CAG lahitaji kuchunguzwa, basi atateua Tume Maalum ambayo itakuwa na Mwenyekiti na Wajumbe wengine wasiopungua wawili.
Mwenyekiti na angalau nusu ya wajumbe wengine wa tume hiyo itabidi wawe watu ambao ni Majaji au watu waliopata kuwa Majaji wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufani katika nchi yoyote iliyomo kwenye Jumuiya ya Madola.
Iwapo Tume itamshauri rais kwamba huyo CAG aondolewe k

Comments