Benki ya Dunia (WB) inakopesha fedha kwenye nchi za dunia ya tatu kwa ajili ya kuratibu na kuendeleza miradi ambayo inahitajika kwa manufaa ya nchi ‘wahisani’ a.k.a nchi wadhamini. WB inapowezesha kifedha miradi ambayo haina tija wala manufaa yeyote kwa wakazi wa eneo husika; utambue kuwa na uchumi wa eneo hilo unazoroteshwa.
International Monetary Fund (IMF) wanakuja kama mwokozi pale ambapo fedha zilizo tolewa na (WB) zinapofanya kile kilicho kusudiwa, ambacho ni kuuzorotesha uchumi wa nchi husika na wakati huohuo kuzifanya fedha hizo kuwa ni mzigo usio lipika. (IMF) wanapoingia wanatoa mikopo zaidi na hivyo kuongeza deni lisilo lipika kuwa ni kubwa zaidi, lakini mikopo hiyo inakuja na masharti, kama vile ‘uongozi mzuri’, ‘utawala bora,’ ‘haki za mashoga,’ ‘kutoa aridhi na rasilimali nyingine kwa wawekezaji.’
Kuna kile kinacho fahamika kama ‘free trade’,
ambacho kinahusisha makubaliano ya kimataifa kama vile GATT, NAFTA na APEC ambayo yanachukuliwa kama ni kitu kizuri na bora zaidi na mawakala wa Illuminanti, sababu ni mfano ‘mzuri’ wa mashirikiano ya kimataifa. Lakini wasicho kijua mabilioni ya watu ni kuwa ‘free trade’ inaigeuza dunia nzima kuwa tegemezi wa bidhaa kutoka kwenye mashirika ‘mahususi’ ya kimataifa.
Majina makubwa kwenye biashara kama vile NIKE, GAP, PEPSI, TN, LEVIS’S, REEBOK, CALVIN KLEIN, COCA COLA, ADIDAS, MC DONALD, na mengine na mengine. Haya ni mashirika ya kimataifa ambayo bidhaa zake zipo kwenye kila kona na uchochoro wa dunia hii, bidhaa zake ndiyo bidhaa unazozikuta kwenye maduka makubwa kama ‘Mall’ na vijiduka vidogo vya kina ‘Mangi’. Maana yake ni kuwa bidhaa za wazawa wa eneo husika hazitauzika, viwanda vyao na teknolojia yao itadumaa na wataishia kuzalisha malighafi zitakazo nunuliwa kwa bei ya chini na mashirika hayo, ambayo baadaye watarudi na bidhaa watakayo uza bei kubwa maradufu kushinda malighafi walizo chukua.
Mbaya zaidi ‘free trade’ inaondoa zoezi la kutoza ushuru baina ya nchi washirika, bidhaa za ndani zinapoteza ulinzi dhidi ya bidhaa kutoka nje kwa kutotozwa ushuru. Hivyo vijinchi vyetu katu havitakaa vinyanyuke kiviwanda wala teknolojia, siku zote tutaendelea kuwa tegemezi kwenye bidhaa za mashirika ya kimataifa. Kwa vile hatutaweza kulipa deni la (WB) na (IMF) wameongeza mzigo wa deni hilo, aridhi yetu inakuwa ni mali yao, mali ya mashirika ya kimataifa kuitumia watakavyo. WAKO WAPI WASOMI WANAO SEMA AFRIKA TULIPEWA UHURU? MBONA ARIDHI ZINAKWENDA? MASHIMO YA MADINI NA VISIMA VYA MAFUTA VINAKWENDA?
Chakula nacho ni nukta ya muhimu kwenye hili. Sasa yananyanyuka mashirika ya kimataifa yenye sura kama NIKE au ADIDAS, lakini haya si kwenye viatu au nguo; Ila kwenye chakula. Hivi sasa nchi zetu za dunia ya tatu zimekumbwa na mafuriko ya kuangamiza mbegu zetu za asili na kutupatia mbegu za kisasa, tizama posti hii,
Utazisikia serikali zetu, maajenti wao na maajenti wa Illuminanti wakilipigia sana jambo hili zumari, na kulipigia debe mno, kwamba hatma yetu suluhisho la njaa zetu, ni mbegu za kisasa. Loh! Tumekuwa ‘wajinga’ na ‘wapumbavu’ wa mwisho, tunapewa kichupa chenye rangi ya dhahabu na sisi tunatoa dhahabu halisi!!! Kwa utaratibu huu sasa, 90% ya chakula wanacho kula walimwengu kipo kwenye mikono ya mashirika ya kimataifa machache yenye kuhesabika. Huu ni msiba juu ya msiba.
KAMA UNAZO MBEGU ZAKO ZA ASILI ZITUNZE NA ENDELEA KUZALISHA KWA MBEGU HIZO NA WARITHISHE WANAO, KAMA UNAVYO WARITHISHA MALI ZINGINE, SABABU SIKU ITAFIKA, DUNIA NZIMA HAKUTAKUWA NA HATA MBEGU Mg YA ASILI
USIKOSE SEHEMU YA PILI YA MAKALA HII.
Comments
Post a Comment