IMF: SERIKALI YA TANZANIA YAPINGA UCHAPUSHAJI WA RIPOTI YA UCHUMI WAKE.



Serikali ya Tanzania imedaiwa kukataa kuruhusu uchapishaji wa ripoti ya hazina ya fedha duniani IMF kuhusu hali ya kiuchumi ya taifa hilo la Afrika mashariki hatua ambayo huenda ikaathiri uwekezaji na misaada kuingia nchini humo.

Kupitia kifungu cha nne cha makubaliano, IMF inaruhusiwa kuchunguza uchumi , hali ya kifedha na sera ya ubadilishanaji wa fedha ya wanachama wake ili kuhakikisha kuwa mfumo wake wa kifedha unatekelezwa bila matatizo yoyote.

Hatua hiyo inashirikisha ziara ya maafisa wa IMF ya kila mwaka katika taifa hilo ili kuangazia data mbali na kufanya vikao na serikali pamoja na maafisa wa benki kuu.

Baadaye wanatoa ripoti kwa bodi kuu, ambayo hutoa maoni yake kwa serikali na kuchapisha ripoti hiyo katika tovuti yake baada ya kupata ruhusa kutoka kwa taifa hilo.


''Mnamo tarehe 18 mwezi Machi , bodi kuu ya shirika hilo la fedha duniani ilikamilisha ripoti hiyo ya baada ya kufanya vikao na maafisa wa serikali ya Tanzania'', ilisema IMF katika taarifa iliotumwa kupitia barua pepe siku ya Jumatano.

Mamlaka haijaruhusu kuchapishwa kwa ripoti hiyo.

Katika ripoti hiyo IMF imetaja ukuwaji wa kiwango cha chini cha asililimi 4 cha uchumi mwaka huu kutoka asilimia 6.6 mwaka 2018, kulingana na makadirio yaliochapishwa mapema mwaka huu.

Taifa hilo lenye utajiri wa madini na gesi katika eneo la Afrika mashariki ni la pili kwa ukubwa wa kiuchumi baada ya Kenya .

Uongozi wa rais Pombe Magufuli
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amepongezwa sana katika vita vyake dhidi ya ufisadi na utenda kazi wa serikali mbali na kukosolewa kwa kuweka sera ambazo wawekezaji wanasema zitaathiri taifa hilo ambalo ni la nne kwa uzalishaji wa dhahabu.

Mwaka 2017, alitaka kampuni ya uchambaji madini ya Acacia Mining Limited kulipia serikali kodi yenye thamani ya $190.

Mwaka huu aliamua kwamba serikali itamiliki kiwango kikubwa cha hisa za kampuni ya Bharti Airtel- baada ya kudai kwamba kampuni hiyo ya mawasiliano ilijipatia hisa hizo kinyume na sheria.

Uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja ulianguka kwa asilimia 2 katika ukuaji wa kichumi wa taifa hilo 2017 kutoka asilimia 5 2014, kulingana na benki ya dunia.

Makadirio hayo yalikuwa tofauti na yale yaliotolewa na serikali kwamba uchumi utakuwa kwa asilimia 7.3 mwaka 2019.

Msemaji wa wizara ya fedha nchini Tanzania hakutoa tamko lolote kufuatia ombi la shirika la habari la Reuters akidai kwamba alikuwa katika mkutano.

Comments