KAKA WA OMAR AL BASHIR NAO CHINI YA ULINZI.


Image may contain: 1 person, glasses and beard















Baraza la Mpito la Kijeshi nchini Sudan limethibitisha kuwashikilia
ndugu wawili wa rais aliyepinduliwa Omar al Bashir.
Msemaji wa Baraza la Mpito la Kijeshi Shams Al Din Kabashi amewataja kaka wa Al Bashir wanaowashikilia ni Abdullah Hassan Al Bashir na Alabas Hassan Al Bashir ambao kwa sasa wapo kizuizini.
Tangazo hilo limekuja muda mchache baada ya Mamlaka nchini Sudan kuthibitisha Al Bashir amehamishwa kutoka kuzuizi cha nyumbani na badala yake kwa sasa anashikiliwa akiwa Gereza la Kobar.

Comments