Kiongozi mkuu wa Iran amteua Bw. Salami kuwa kamanda wa Jeshi la ulinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran. #Duniayako



Shirika la habari la Iran Tasnim limesema kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei ametangaza kumteua Bw. Hossein Salami kuchukua nafasi ya Bw. Mohammad Ali Jafari na kuwa kamanda wa Jeshi la ulinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC).


Bw. Salami aliyezaliwa mwaka 1960 mkoani Isfahan, katikati ya Iran, alijiunga na Jeshi la ulinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran mwaka 1980, baada ya vita kati ya Iran na Iraq . Kabla ya kuchukua nafasi ya Jafari, alikuwa naibu kamanda wa jeshi la IRGC.

Jeshi la IRGC lilianzishwa mwaka 1979, na limeshirikiana na jeshi la ulinzi la Iran na kuwa nguvu kuu ya ulinzi wa nchi.

Comments