MAVAZI YA KUZIBA USO MARUFUKU SRI LANKA



Sri Lanka imepiga marufuku watu kujifunika uso hadharani kufuatia mashambulio ya kujitoa muhanga katika sikukuu ya Pasaka yaliosababisha vifo vya watu zaidi 250 na mamia wengine kujeruhiwa.



Rais Maithripala Sirisena ametangaza hatua hiyo ikiwa ni sehemu ya sheria ya dharura kuidhinisha marufuku hiyo kuanzia leo Jumatatu.

Kupitia ofisi ya Rais Sirisena imesema, kitambaa chochote kinachofunika "na kuzuia mtu kutambulika " kitapigwa marufuku kuhakikisha usalama.

Viongozi wa dini ya kiislamu wameshutumu uamuzi huo, licha ya kwamba vazi la Niqab na burka yanayovaliwa na wanawake wa kiislamu  hayakutajwa kama ndiyo yaliodhamiriwa katika marufuku hiyo.

Comments