MUHIMBILI WAMPOKEA BINTI ANAYESUMBULIWA NA KIDONDA KIKUBWA MGONGONI.

Image may contain: 3 people
MUHIMBILI WAMPOKEA BINTI ANAYESUMBULIWA NA KIDONDA KIKUBWA MGONGONI.
Mariam Rajab (25), mkazi wa kitongji cha Inung'una mkoani Singida, aliyeteseka kwa muda mrefu na kidonda mgongoni, ambaye video yake ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii akiomba msaada wa matibabu, hatimaye amepokelewa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), saa sita usiku wa jana, Jumatano.
Mariam amepokelewa katika Idara ya Magonjwa ya Dharura, ambapo kwa sasa anaendelea kufanyiwa vipimo vya awali na kisha atalazwa, ili aweze kuonana na jopo la madaktari bingwa wa upasuaji kwa ajili ya kupatiwa matatibu zaidi.

Msemaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Algaesha ameweka wazi kuwa matibabu ya mgonjwa huyo yatagharimiwa na hospitali hiyo.
Kupitia video yake iliyosambaa katika mitandao ya kijamii, binti huyo alijieleza namna anavyoteseka na kidonda hicho.
“Mimi naitwa Mariam Rajabu naishi katika Mkoa wa Singida, Mtaa wa Mnung’una naishi katika familia ya kimasikini, wazazi wangu hawana uwezo wa kunisaidia tatizo langu, tatizo ambalo ninalo, tatizo lenyewe ambalo ninalo ni kidonda ambacho kipo hapa mgongoni, naombeni Watanzania wenzangu muweze kunisaidia niweze kwenda hospitali ya Muhimbili ili niweze kupata matibabu.Sina cha kuwalipa bali Mungu atawalipa, asanteni”
Baada ya kuonekana kwa video hiyo, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu aliuagiza uongozi wa MNH kumtafuta Mariam popote alipo ili apelekwe hospitalini hapo kwa ajili uchunguzi na matibabu.
Mariam ameletwa Muhimbili kwa gari la wagonjwa kutoka mkoani Singida, lililoanza safari yake saa 8:00 mchana jana.

Comments