Rais John Magufuli amechangia shilingi milioni mbili kwaajili ya kununua mashine ya kudurufu nakala pamoja na kuvuta umeme katika Shule ya Msingi Ileje iliyopo Rungwe mkoani Mbeya na kutoa siku kumi kukamilika kwa zoezi hilo.
Rais Magufuli ametoa kiasi hicho baada ya wanafunzi wa shule hiyo kumlalamikia kutokuwa na umeme na kifaa hicho katika shule yao, alipokuwa wilayani humo kuzindua kiwanda cha parachichi katika muendelezo wa ziara yake ya siku nane mkoani Mbeya.
Comments
Post a Comment