Serikali ya Tanzania imesema kwamba haitapiga marufuku matumizi ya kucha bandia na kope bandia baada ya mamlaka ya chakula na madawa nchini humo (TFDA) kuthibitisha kwamba hakuna hatari ya kutumia bidhaa hizo.
Waziri wa ulinzi Hussein Mwinyi, ambaye pia ni daktari- aliambia wabunge jijini Dodoma kwamba utafiti uliofanywa na TFDA umebaini kuwa hakuna hatari yoyote ya kutumia kucha bandia au kope bandia.
Hatua ya serikali ya Tanzania kutopiga marufuku kucha bandia na kope bandia inajiri miezi sita baada ya Spika wa bunge la taifa hilo Job Ndugai kupiga marufuku wabunge dhidi ya kuingia bungeni wakiwa wamevalia kope bandia na kucha bandia.
Comments
Post a Comment