TANZANIA: MCHUNGAJI AKUTWA NA TUHUMA ZA DAWA ZA KULEVYA.



Raia watatu wa kigeni akiwemo anayejiita mchungaji kutoka nchini Nigeria Hemry Ozoemena Ugwuanyi wananaswa na kitengo cha kuzuia na kupambana na dawa za kulevya cha nchini Tanzania wakiwa na kilo 15 za dawa za Heroine.


Hatua hii ya mchungaji huyu kunaswa akiwa na dawa za kulevya ni gumzo katika makundi mbali mbali nchini humo na hasa ukizingatia hadhi na uaminifu mkubwa ambao wamekuwa wakipewa wachungaji na makaasisi.

Mchungaji huyo alikamatwa mara baada ya raia mwingine wa kigeni nchini humo kukamatwa katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na kutoa taarifa kuwa mchungaji Hemry Ozoemena Ugwuanyi ndiye aliyempa mzigo wa dawa za kulevya kusafirisha kwenda Poland.

Huu ni mwaka wa tatu tangu mchungaji huyo aanze kufanya shughuli zake za uchungaji nchini Tanzania.

Mchungaji Raphael Kitime ni mchungaji wa kanisa la Tanzania Assemblis of God anasema yanayotokea yanaharibu huduma ya kichungaji lakini hata maandiko yako wazi kuwa watu wajihadhari na manabii wa uongo.

Cha msingi ni serikali kuwa makini katika kusajili haya makanisa na wanaoumia ni raia.

Hao watu ni manabii wa uongo na wanataka kuwaumiza raia na kuwaibia fedha zao hivyo hata jamii wanapaswa kuwa makini zaidi. #Duniayako

Comments