VAN DIJK ACHUKUA UCHEZAJI BORA ENGLAND, TUZO ZA PFA



Beki wa Liverpool, Virgil van Dijk ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa nchini England (PFA) katika hafla iliyofanyika usiku wa jana kwenye ukumbi wa Grosvenor House jijini London.


Beki huyo Mholanzi mwenye umri wa miaka 27 amewashinda Raheem Sterling, Bernardo Silva, Sergio Aguero (Manchester City) Sadio Mane (Liverpool) na Eden Hazard (Chelsea).

Van Dijk amerithi tuzo ya mchezaji mwenzake wa Liverpool Mohamed Salah aliyeshinda tuzo hiyo katika msimu wa 2017/18 na ni beki wa kwanza kushinda tuzo hiyo tangu msimu wa 200/05 ilipokwenda kwa John Terry.

Amesajiliwa Januari 2018 akitokea Southampton kwa paundi milioni 75 na amekuwa nguzo muhimu katika safu ya ulinzi ya Liverpool akiiwezesha kucheza mechi 19 bila kuruhusu bao (clean sheets), na kushinda mechi 28 kati ya 36 ilizocheza msimu huu.

Mbali na ulinzi, Van Dijk pia amefunga mabao matatu na kutoa assist mbili akicheza mechi zote kwenye ligi msimu huu.

Wachezaji 11 wanaounda timu bora ya msimu ya #PFA ni Ederson, Alexander Anold, Robertson, Laporte, Van Dijk, Fernandinho, Barnardo Silva, Pogba, Aguero, Sterling, Mane.


Comments