Mwanamke mmoja raia wa Malawi asiyekuwa muathirika wa Ukimwi ambaye alimeza dawa za kutibu makali ya ugonjwa wa ukimwi kwa muda wa miaka mitatu baada ya kupewa matokeo yasiyokuwa sahihi ya ugonjwa huo kuwa ameathirika sasa anatarajia kulipwa fidia na serikali ya taifa hilo.
Mwanamke huyo kwa jina Agnes Jumbe alipewa matokeo ya kupotosha na kuwekwa kwenye mpango wa kumeza dawa za ARV baada ya kupimwa katika hospitali ya umma mwaka wa 2014. Mawakili wake waliambia mahakama ya Lilongwe kwamba mwanamke huyo alipitia wakati mgumu mno katika kipindi hicho ikiwemo kutalakiwa na mume wake. Jaji Ivy Kamanga ambaye alikuwa akiwakilisha serikali alikubali kuwa serikali italipa mwanamke huyo.
Comments
Post a Comment