CUF YAANZA KUIBOMOA CHADEMA



CHADEMA VIPANDE VIPANDA  *WILFRED LWAKATARE* NA *SILVESTER KASULUMBAI* AJIUNGA RASMI NA CUF .

.1- Shangwe , Vigeregere na Nderemo Zalipuka Buguruni Wanachama na Wafuasi wa  CUF WATETEMA kwa furaha.

2-  Uzinduzi wa  SERA ni  tarehe 22/6/2019 Wabunge Wengine na Madiwami Kupokewa.Diamond Jubilee

3 - Waliokuwa Wanakerwa na Ubaguzi wa MAALIM  SEIFU Waanza Kurejea CUF.

4- Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa , Vijiji na Vitongoji #CUF kuvuna  Msururu Mrefu wa Viongozi Makini wa Kisisia Unakuja

.

*MWANDIDHI David Maphone.*
..

Chama cha wanananchi CUF Jana 8/6/2019 Kimefanya KUFURU kwa kile wanachokiita wao Kutest mitambo  kabla ya tarehe 22/6/2019 watakapozindua SERA ya Chama hicho pamoja na kuwapokea wanachama Wengine Wapya na  Viongozi Mbali Mbali Kutoka  Vyama Vingine  Vya Siasa Wakiwemo Madiwani na Wabunge .

 * Yote haya Yanatajwa Kuwa ni Maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi MKUU 2020.

Katika Mkutano huo uliofanyika Buguruni jijini Dsm  Ukiongozwa na Mwenyekiti wa  Chama  Prof Ibrahim LIPUMBA  wanachama na wapenzi was Chama hicho walipuka kwa furaha baada ya kuwaona MBUNGE wa  BUKOBA MJINI (CHADEMA)  Mheshimiwa Wilfred LWAKATARE Wakiongozana na MBUNGE wa  MASWA (CHADEMA)  2010/2015  Mheshimiwa Silvester KASULUMBAI  akikabidhiwa Kadi na Mchumi wa  Dunia Prof Ibrahim LIPUMBA.

 Akizungumza  kwenye tukio hilo  mwenyekiti wa  CUF amesema Leo  sio siku  ya kupokea Vigogo kutoka vyama mbalimbali Shughuli hii itafanyika Diamond Jubilee tarehe 22/12/2019 wanachama mjitokeze kwa wingi  Chama cha CUF sasa kimezaliwa Upya.

Naye  Naibu Katibu MKUU Magdalena Sakaya  amesema Leo hatuwezi kuwapa fursa wageni wetu kuongea Najua wengi wenu mnahamu sana ya kumsikiliza Mbunge Mwenzangu LWAKATARE na KASULIMBAI lakini  mtuvumilie tutawapa nafasi ya kuzungumza nanyi  tarehe 22/6/2019 tunakwenda kujenga Chama kimya .

Wanachama mbalimbali walipata fursa ya kupiga PICHA na LWAKATARE na KASULUMBAI huku viongoxi hao wakiahidi Makubwa ndani ya CUF na kurejesha heshima baada ya kuondoka kwa (DIKTETA MWENYE NDEVU CHAKAVU).


Comments