HATIMA YA CHAMA CHA ACT- WAZALENDO IPO MIKONONI MWA OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI.



KUKURUKA ZA ACT-WAZALENDO KUGAWANA VYEO WAKATI MAAMUZI YA BARUA YA NIA YA OFISI YA MSAJILI WA VYAMA HAYAJATOLEWA NI HADAA ZA KISIASA KWA WATANZANIA.


1 Act Wazalendo  yauzwa rasmi kwa  Maalim Self na kutimiza lengo lake la kukiteka chama hicho cha siasa kupitia mgawanyo wa  madaraka uliotangazwa.

2.  Mkakati wa kupeana vyeo kwa  lengo la  kuwaongezea thamani viongozi ili chama kitakapofutwa wapekelewe kwenye vyama  vingine kama viongozi.

Ofsi ya Msajili wa vyama vya siasa nchini iliwaandikia barua ya nia ya kukifuta  chama cha Act Wazalendo yenye kumbukumbu HA322/362/20/98 ya Machi 25 kuwataka kujibu hoja mbalimbali ikiwemo kutowasilisha hesabu za ukaguzi za 2013/2014 hatua inayokiuka sheria ya vyama vya siasa sura ya 258.

Chama cha Act Wazalendo wiki mbili kabla ya muda waliopewa na Ofisi ya Msajili  kwisha walitangaza kupeleka majibu yao kwa Msajili ili Maamuzi ya Msajili yaweze kutolewa kwa mujibu wa Sheria.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa na wale wa masuala ya Kisheria wanakubaliana kwa pamoja kwamba ikiwa sheria zitachukua mkondo wake chama cha Act- Wazalendo kina nafasi finyu sana kusalimika na adhabu ya kufutwa kutokana na aina ya Makosa na ushahidi wa wazi uliopo.

.

TUHUMA ZA ACT WAZALENDO,
.

.Chama cha Act Wazalendo kinakabiliwa na Makosa matatu (3 ) ya uvunjifu wa Sheria za vyama ya mwaka 1992 iliyofanyiwa Marekebisho mwaka 2019.

 (a)Act Wazalendo wamevunja  Sheria ya vyama Kifungu namba  18 (3) na (4) Sheria ya vyama Sura namba 258 ya Mwaka 1992 iliyofanyiwa Marekebisho mwaka 2019.kwa kutenda Kosa la kushindwa kupeleka Hesabu kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kinyume na Kifungu hicho.

(b) Act  Wazalendo wametenda Kosa la kuchoma MOTO bendera za chama cha wananchi CUF kinyume na sheria ya vyama Kifungu namba 11C cha Sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 Iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.

 (c) Act -Wazalendo wametenda Kosa la kutumia DINI kwa malengo ya Kisiasa [Takbira] kinyume na Masharti ya Usajili kwa mujibu wa Kifungu namba  9(1)(c) cha Sheria ya vyama vya siasa ya Mwaka 1992 iliyofanyiwa Marekebisho Mwaka 2019.

Makosa yote tajwa hapo juu yamefanyika mchana kweupeeee tena kwa mbwembwe na kila Mtanzania alikuwa shuhuda  wa tukio hilo,  kutoka siku Maalim Self atangaze kujiunga Act Wazalendo, Picha mnato na video Clip zinaonyesha kufanyika kwa tukio hilo ililochukua wiki mbili mfurulizo Tanzania Bara na Zanzibar kibaya zaidi Bendera ya chama ilikuwa ikipandishwa kwa DUA Maalumu ( TAKBIRA ) na sio (TAKBIR ) kama inavyopotoshwa na Zitto Kabwe na kusababisha Umoja wa vijana wa Shura ya Maimamu mkoa wa D'salaam kukemea.

Ukiwa mwanasiasa unayejitambua unawezaje kufikiria kugawana vyeo kwa chama kiko ICU hakijulikani hatima yake?

Mosi, mgawanyo huu wa vyeo ni Ujanja wa Zitto Kabwe na Maalim Self na wenzake kwenye kipindi hiki ni  kutafuta Jukwaa (Platform) ya kuzungumza na kuandika kwenye Mitandao kwa baada ya Chama chao kufutwa maana kwa sasa Mbarala, Bashange, Jussa, Bimani wangezungumza kama nani

Pili, Wanahitaji kujiongezea THAMANI chama chao kikifutwa kule waendako wapokelewe kwa vyeo vyao ili kuendeleza utamaduni wao wa kutukana viongozi wa kisiasa , Serikali na wanaowachukia,

Tatu, Mgawanyo huu wa Madaraka ni kama maandalizi ya Zitto  kwajili ya kwenda Mahakamani hivyo wale waliokuwa wakifungua makesi hadi (39) na kuandika kwenye Mitandao ndio hao hao waliozawadiwa vyao hewa.

Mgawanyo huu wa vyeo ni ujanja wa Zitto ili kuwaongezea THAMANI viongozi wake baada ya kufutwa kwa chama chake kwa sababu Zitto hana ujinga wa kushindwa kufahamu kuwa Safari hii kakutana na kisiki Wallah Wallah hawezi kuchomoka labda pawepo na upendeleo au msamaha !!.

Lakini kingine ukisoma Katiba ya Act Wazalendo unabaki ukishangaa vyeo walivyopeana havionekani kwenye Katiba ya Act Wazalendo hakuna tofauti na yale makamati ya uongozi yaliyokuwa yakiundwa na Maalim Self akiwa



Mchambuzi David Maphone

Comments