INAWEZEKANAJE LIPUMBA AWE MSALITI KWA KUMKATAA LOWASSA KWA KUWA BADO ALIAMINI NI MWANA- CCM MTIIFU NA FISADI.
"TATHMINI YA UCHAGUZI MKUU 2015:
Anaandika Eng. Mohamed M. Ngulangwa.
" Tuna Imani na Lowassaaa! Oyaa Oyaa Oyaaa".
Hizo ni Shamra Shamra zilizomkaribisha aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Awamu ya NNE (4) kwenye Ukumbi wa Mkutano wao huko Dodoma, SAA chache baada ya kukatwa kwa Edward Ngoyai LOWASSA. Hapa wanakutana kuchuja miongoni mwa majina matano (5) yaliyobaki, ili wapate majina matatu yatakayopigiwa Kura ili apatikane Mgombea wa Urais kupitia CCM.
Upepo Ukumbini haukuwa mzuri na wajumbe walidhihirisha kutoridhishwa na hatua ya kukatwa kwa KADA MTIIFU WA NYAKATI ZOTE WA CCM na MTU muhimu kwa USALAMA wa TAIFA, Mheshimiwa Edward LOWASSA. Kikwete jasho lilimtoka katika kutuliza mzuka wa wajumbe.
MAGUFULI ACHANGAMKIA FURSA:
Hali ya taharuki ikiendelea Ukumbini huku wajumbe kadhaa wakiwa wamesimama na kupiga kelele, pembeni anaonekana mmoja wa Wagombea watano (5) waliopitishwa, Dr JP Magufuli akiteta jambo na LOWASSA.
Bila shaka Magufuli alikuwa anajaribu 'KWA MAFANIKIO' kumsihi LOWASSA awatulize wapambe wake ili ' JAMBO LIPITE' na huenda aliomba wapambe wake wahamishie KURA ZAO KWAKE.
Ni imani yangu kwamba LOWASSA alihakikishiwa 'makubwa' kwani Mara baada ya wawili hawa kuteta, wajumbe wote wakarejea kwenye nafasi zao na Utulivu ukarejea Ukumbini. Hatma ya Utulivu huu ni kufanikisha kuchuja wagombea kuwapata watatu kabla ya kupiga Kura na kumpitisha Magufuli ( Hapa sikusudii kueleza Yale yaliyosambaa kwamba aliyeshinda ni 'mama mmoja').
LOWASSA APEWA JUKUMU ZITTO:
Kutokana na Hali ya Kisiasa iliyokuwepo 2015, iliyotiwa CHACHU na BUNGE LA KATIBA, ambalo ni CHIMBUKO LA UKAWA, hali ilikuwa mbaya sana kwa CCM.
Ni UKWELI usiopingika kwamba Magufuli hakuonekana kuwa na UBAVU wa kupambana na DR. SLAA, ambaye alishapigiwa Chapuo kuwa 'MGOMBEA WA UKAWA'. CCM iliona kaburi lake kupitia Uchaguzi huu. Hakukuwa na namna ya kupambana na Nguvu hii ya Upinzani zaidi ya kuwavuruga. LOWASSA akatolewa kwa mkopo ili azuie Dr Slaa kugombea, ili kuzuia nchi kutwaliwa na Upinzani.
CCM YANUSURU URAIS KWA MABILIONI NA KUGAWA VITI VYA MUDA VYA UBUNGE NA UDIWANI:
Ili kufanikisha Mpango wa kuzuia UKAWA kuichukua nchi, LOWASSA akatinga Upinzani na kutumia NGUVU YA PESA KUWAGAWA UKAWA. Wafanyabiashara wakapiga hesabu, wakaona ' URAIS SI KITU'. Wakatupa Ajenda ya UKAWA na kuamua kumtanguliza MPINZANI WA UKAWA KWENYE BUNGE LA KATIBA.
MPANGO WA CCM WATIMIA -VIONGOZI WA UKAWA WAPARAGANYIKA:
Freeman Mbowe, Prof. Ibrahim Lipumba, Dr W. Slaa, Maalim Seif, Mbatia, Makaidi na viongozi wengine wa UKAWA walimpokea LOWASSA kama mwanachama mpya wa Chadema. Hata hivyo walitofautiana juu ya hadhi yake kuhusu Kugombea Urais kama ifuatavyo:
(a) Prof. Lipumba na Dr. W. Slaa waliamini LOWASSA hakutosha kuwa Mgombea Urais kwa kashfa ya Ufisadi na pia kutotosha kuibeba Agenda ya Katiba ya Wananchi, ambayo ndiyo sababu ya UKAWA. Pia LOWASSA hakuaminika kutoka CCM kwa dhati.
(b) Mbowe na Maalim Seif walijali tu maslahi ya masurufu na kutojali walichokiongea kwa miaka 8 ( 2007 - 2015) kuhusu Ufisadi wa LOWASSA.
LOWASSA AWA NYOTA WA MCHEZO:
LOWASSA alifanikiwa kuzuia UKAWA kusimamisha Mgombea Urais. Hilo ni jambo muhimu zaidi kwa CCM. Kufanikiwa kwa LOWASSA kupo katika maeneo yafuatayo:-
1.Lowassa alifanikiwa kuzuia UKAWA kusimamisha Mgombea Urais mwenye hadhi ya kubeba Agenda ya KATIBA YA WANANCHI na asiye na Makandokando na Kashfa ya UFISADI. Lowassa alikuwa mpinzani Mkubwa wa mapambano ya Kudai Katiba ya Wananchi, iliyokubaliana na RASIMU YA KATIBA YA JAJI WARIOBA.
2. Lowassa alifanikiwa kuwacheza Shere Wapinzani kwenye Majukwaa ya Kampeni kwa kudiriki kutamka " CCM Oyee" zaidi ya Mara moja. Isitoshe, alitumia hadi pungufu ya dakika tatu (3) kuhutubia jukwaani, kutokana na kilichodaiwa kuwa ni maradhi. Maradhi hayo yalitoweka Mara baada ya Uchaguzi Mkuu.
3. Lowassa alifanikiwa kuwalaghai Watanzania kupitia Mkakati huu aliotumwa kuutek
Comments
Post a Comment