KUVUNJA SHERIA HALALI ZA VYAMA VYA SIASA NCHINI HAKUJAWAHI KUKIACHA CHA CHOCHOTE SALAMA.
.
Kutokana na UVUNJIFU wa sharia ya vyama vya siasa mpaka sasa vyama vipatavyo Sita (6) Vimekwisha FUTWA na kuondolewa kabisa katika Orodha ya Daftari la MSAJILI wa vyama vya siasa Nchini, huku ndiko kunakoitwa Kisheria ( KUKIUKA MASHARTI YA USAJILI ).
Kuendesha vyama au shughuli za Kisiasa Duniani Kote kuna Masharti yake yanayopaswa Kuzingatiwa kwa kila chama cha siasa, tofauti ya Chama cha siasa na vyama vya NGOMA ni Kubwa mno, wakati Madhara ya Chama cha siasa ni Makubwa kutokana na kibali cha Kuendesha Shughuli zake ni Nchi nzima na kugusa maisha ya watu Kwa kila nyanja.
Chama cha Act wazalendo pamoja na kuwa kinapokea Ruzuku isiyozidi Tsh 3,500,000 / wameshindwa kupeleka Hesabu za mwaka 2013/2014 Kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Kinyume na Sheria Kifungu namba 18 (3) na (4) Sura namba 258 ya mwaka 1992 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 .
Kwa kosa kama hili chama hiki kinabakiaje kwenye Daftari la Orodhs ya vyama vya siasa ? Na kama kinabakia kwanini vyama Vingine Sita (6) Vilifutwa Kwa kuvunja Sheria Kama ACT Wazalendo? Au ndio tuseme Sheria hii IPO kwajili ya vyama Vingine sio Act Wazalendo?
Hili ni kosa moja TU, kati ya makosa matatu yaliyoainishwa kwenye Barua ya NIA ya MSAJILI wa vyama kukifuta chama Cha Act Wazalendo, Chama hiki kipo kwrenye ICU chumba cha wagonjwa Mahututi kikipumulia Machine unawezaje kupoteza pesa na muda kujiunga kabla ya Kusubiri HATIMA yake ( Maamuzi ya MSAJILI) ?
USIKOSE SEHEMU YA TATU KUSOMA KOSA NAMBA MBILI, "HATIMA YA ACT MIKONONI MWA MSAJILI"
MWANDISHI David Maphone.
0714304970
DSM Tanzania .
Comments
Post a Comment