WAZIRI NDALICHAKO AZIPONGEZA SHULE ZA FEDHA KWA KUHAMASISHA MASOMO YA SAYANSI NA HISABATI



Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameupongeza uongozi wa shule za Feza kwa kuhamasisha masomo ya sayansi na hesabu  kwa kuwashirikisha wanafunzi katika mashindano ya kimataifa.


Akizungumza katika mahafari ya 13 ya kidato cha sita ya shule hizo yaiiyofanyika Jijini Dar es Salaam Prof Ndalichako amesema kuhamasisha masomo hayo ni kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli za kuipeleka Tanzania katika Uchumi wa kati  kupitia viwanda.

"Hatuwezi kufanikiwa kuwa na uchumi wa kati unaojengwa na viwanda kama hatujawekeza na kuhamasisha elimu ya  sayansi, teknolojia na ubunifu kwa  vijana wetu" amesisitiza Ndalichako

Aidha, Prof. Ndalichako amesema serikali  inaendelea kuboresha mazingira katika vyuo vikuu ili kuwawezesha vijana wa Kitanzania wanaojiunga na vyuo hivyo kupata elimu bora.

Amewataka wanafunzi waliomaliza kidato cha sita kuitumia vyema elimu waliopata katika kushiriki masuala mbalimbali ya kimaendeleo na kijamii. Huku akiwataka  kubadilisha changamoto mbalimbali wanaziona katika jamii kuwa fursa na  kuja na njia mbalimbali za kuisaidia kuzitatua badala ya kuwa walalamikaji.

"elimu nzuri miliyopata iwasaidie kuona fursa zaidi  badala ya kuona matatizo zaidi, sehemu mnayoiona changamoto iwasaidie kuwa wabunifu katika kuleta mabadiliko katika jamii inayowazunguka" amesema Waziri Ndalichako.

Naye Mkurugenzi wa Shule za Feza Ibrahim Yunus amesema katika kuunga mkono jitihada za serikali kutoa elimu bure, shule zake zimekuwa zikitoa ufadhili katika shule za umma zinazowazunguka ambapo mpaka sasa wanafadhili wanafunzi 184 kwa kuwapatia kiasi cha shilingi 250,000 kila mmoja kwa ajili ya kununua vifaa vya kujifunzia na kujikimu.

Mwakilishi wa wazazi wa wa wanafunzi hao Prof. Mtui ambae pia ni Naibu Makamu Mkuu Chuo Kikuu Mbeya  ameishukuru Serikali ya awamu ya tano  kwa kuweka mazingira bora  ya uwekezaji katika elimu hivyo kuwezesha vijana wa kitanzania kupata elimu bora na kwa viwango vya kimataifa.

Comments