MJUE MH SHAMSIYA AZIZI MTAMBA NA SAFARI YAKE KISIASA












Shamsia Azizi ni mtoto wa kwanza akiwa amezaliwa katika hospital ya Ligula Kata  Manispaa ya  Mtwara Mjini tarehe 05/July/1986


ELIMU YAKE

Mh Shamsia Azizi  Elimu yake ya msingi alisomea shule ya Shangani Mtwara Mjini kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 2001 na elimu yake ya Secondary alisomea shule ya Nangwanda Wilaya ya Newala kuanzia mwaka 2002 Hadi mwaka 2005

SAFARI YAKE KISIASA NA KIUONGOZI

Ndugu SHAMSIYA AZIZI MTAMBA alikuwa mwanachama rasmi kwa kuchukua kadi ya chama cha wananchi CUF  mnamo mwaka 2005 akiwa mkaazi na mwananchi wa Mtwara Mjini
Miaka kadhaa baadae aliajiriwa na kuwa mfanyakazi katika shirika la posta na simu Tanzania linalo milikiwa na serekali baadae aliacha kufanya kazi katika shirika la Posta na kuanzisha NGO's iliyokuwa inajulikana kwa jina la  "FAOPA GROUP " akiwa kama msimamizi na mfanya kazi
FAOPA GROUP (FG) ilijikita asilimia 100% katika maudhui ya kutoa Elimu kwa vijana wakike na wakiume yani Psychological Counseling hasa wathirika wote wa kundi tajwa waliokuwa na dalili ama waliokwisha kupata maambukizi ya ugonjwa wa  Ukimwi yani HIV/AID'S hapo ilikuwa ni kati ya mwaka 2010 hadi 2015 hadi.


 Mh.Shamsia akiwa katika harakati za ujenzi wa chama na wakinamama

Kamanda SHAMSIYA AZIZI MTAMBA alianza na kuingia kibaruania rasmi (for a full-time) katika kukitumikia chama cha wananchi CUF sasa akiwa bado kazini hasa kuanzia mwaka 2007 hadi 2009 akiwa shirika LA posta Manispaa  MTWARA MJINI.

Mnamo mwaka 2014 hadi  2015 mwana mama Jasiri Huyu aliingia mzima mzima,kichwa mikono na miguu  yake yote katika chaguzi za serekali za mitaa na vijiji mkoani mtwara manispaa ya mtwara Mjini kuhakikisha wagombea wote S/Mtaa na vijiji watokanao na chama cha wananchi CUF wanashinda kwa kishindo na kunyakuwa ushindi bila kukwama wala kukwamishwa.





 Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 aliingia kikomando katika mapambano hasa akiwanadi wabunge na madiwani watokanao na chama cha wananchi madiwani  hasa akitumia taaluma yake ileile ya FOABA GROUP ya kuwa shawishi na kuwaelimisha rika kubwa la vijana na akina mama mjini na vijijini katika kujitokeza kujiandisha na kupiga kura kwa kuwaunga mkono wagombea wote watokanao na chama cha CUF na wabunge ali fanya kazi kubwa ya kuwaelimisha vijana na wanawake zoezi lake hilo aliweza kuwavuna wakina mama wengi kwa sababu alikuwa msada wao na karibu nao hivyo kupeleka vilio na simanzi katika CCM kitu ambacho HALIMA DENDEGU aliyekuwa mkuu wa mkoa wa mtwara wakati ule  kumsumbua sana kwa vitisho na kumpa rapsha za namna kwa namna  lakini haikuwazuia wakina mama mkoa wa MTWARA hasa manispaa kuamua kufunga kibwebwe kukiunga mkono chama cha CUF pamoja vyama vingine kusimamisha wagombea lakini wanawake walishakwisha kata shauri kukiunga mkono chama cha CUF
Mwaka 2017 miaka miwili baada ya uchaguzi mkuu chama cha wananchi CUF kupitia kamati ya utendaji na baraza kuu lilimtea Ndugu Shamsiya Azizi kuwa mbunge wa viti maalum katika bunge la jamhuri ya muungano kuwakilisha mkoa wa MTWARA katika chombo hiko cha kutunga sheria

Mh.Shamsia akitoa zawadi ya jezi na mipira


Nyota iliendelea kung'aa baada ya mkutano mkuu Taifa wa mwaka 2019 uliofanyikia katika hoteli ya LERKAM DSM kumchagua kwa kura zakishondo mh.Shamsia kuwa mjumbe wa BARAZA KUU LA TAIFA mwanamke wakuchaguliwa kwa kura na kupata kura nyingi zaidi

Baada ya kuwa mbunge kwa kipindi kifupi Mh. SHAMSIYA alianzisha vikundi vya akina mama na vijana kisha kivijengea uwezo kwa kutoa misaada na kuviwezesha vikundi vya wakina mama na vijana kuwawezesha wengi katika soccer kwa kugawa Jezi na Mipira kwa timu za mpira hivyo kuwajengea vijana utimamu wa afya,upendo,na kuwatengenezea miundombinu rahisi ya kujiajiri kwa kupitia mpira wa miguu huyo ndiye Shamsiya

Itaendeleea part2

Comments