CUF-Chama Cha Wananchi kinawatakia Wakristo wote Nchini Siku Kuu njema ya Christmas na kheri ya Mwaka Mpya wa 2020.


SALAMU ZA X MASS NA KHERINYA MWAKA 2020

CUF-Chama Cha Wananchi kinawatakia Wakristo wote Nchini Siku Kuu njema ya Christmas na kheri ya Mwaka Mpya wa 2020.



CUF-Chama Cha Wananchi kinawakumbusha Viongozi wote wa Vyama na Serikali kutumia mafundisho yanayopatika kwenye kumbukizi ya Kuzaliwa kwa Kristo kama mwanzo wa kurejesha upendo na furaha miongoni mwa jamii ya Kitanzania bila kujali itikadi za Kisiasa,Kabila na Dini zetu.

CUF-Chama Cha Wananchi pia kinawatakia Watanzania wote kheri ya Mwaka Mpya na kuwataka Watanzania kujipanga kikamilifu katika kutekeleza majukumu yetu ya ujenzi wa Taifa letu na Familia zetu.

CUF-Chama Cha Wananchi kinautambua Mwaka Mpya wa 2020 kama Mwaka wa Demokrasia na Maridhiano ya Kisiasa hapa Nchini.

Katika kuhakikisha kua hilo linatima ,Viongozi wetu wa Kitaifa Mwezi January 2020 wataanzisha Ziara ijulikanayo Kwa jina la

2020 ni Mwaka wa Demokrasia na Maridhiano.

Oparesheni hii itatambulishwa Nchi nzima Kwa Mikutano ya Ndani ikiwa na lengo la kuonyesha umuhimu wa uwepo wa Demokrasia na Maridhiano kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwezi October 2020.

Pamoja na Salam za Chama za Haki Sawa na Furaha Kwa Wote, pia itafuatiwa na Kauli Mbiu ya Mikutano hiyo ya Ndani ambapo Muendesha Shughuli au Mikutano hiyo atakua akisema 2020 .......

Waliohidhuria watamjibu MWAKA WA DEMOKRADIA NA MARIDHIANOOO

CUF-Chama Cha Wananchi kinaona ipo haja Kwa hali tulionayo kuendeleza Hoja ya kumalizia Kwa mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya ambayo Kwa kiasi kikubwa imeshakaribia kupatikana kwakua Maoni ya Wananchi yamwesha kusanywa na Rasimu ya Kwanza ya Katiba Mpya imeshachapwa.

Uwepo wa Demokrasia na Maridhiano ya Kisiasa ni muhimu sana ili kuweza kufikia upatikanaji wa Katiba Mpya ambapo Ndani yake itapatikana Tume Huru ya Uchaguzi .

Demokrasia na Maridhiano ya Kisiasa ni Nyezo muhimu sio tu katika kufikia Maendeleo ya Kiuchumi na Kisiasa lakini pia huleta upendo,Umoja na hustawisha Amani miongoni mwa Jamii ya Kitanzania.

Mwisho tunawataki Christmas njema na Heri ya Mwaka Mpya.

HAKI SAWA NA FURAHA KWA WATANZANIA WOTE.

2020 NI MWAKA WA DEMOKRASIA NA MARIDHIRIANOOO
......................

Comments