HIZI HAPA DALILI ZA DENGUE
Dengue ni ugonjwa unaoleta homa kwa muda wa siku 2 hadi 7 na huambatana na dalili zifuatazo:
* Kuumwa kwa macho.
* Kuumwa kwa kichwa
.
Maumivu ya misuli na viungo.
* Kutokwa na damu (katika fizi au pua).
* Kukwaruzika kwa urahisi.
Huduma ya nyumbani kwa homa ya Dengue ni:
* Pata vinywaji kwa wingi mfano maji, juisi au chai.
* Tumia dawa za maumivu kupunguza homa.
* Usitumie dawa ya "Aspirin" ama "Ibuprofen"
Nenda hospitali haraka unapoona moja ya dalili za tahadhari. Dalili za tahadhari za kuangalia baada ya homa kuondoka:
* Maumivu makali ya tumbo.
* Kutapika mfululizo.
* Kutokwa damu.
* Ngozi kupauka na kuwa baridi.
*Kudhoofika kwa mwili, usingizi mzito.
* Kizunguzungu, kuzimia.
* Kupumua kwa shida.
Comments
Post a Comment