Idadi ya watu waliofariki nchini Ufilipino jana (Alhamisi) baada ya dhoruba Phanfone kuzuka katika maeneo ya kati ya nchi hiyo imeongezeka hadi 21

Idadi ya watu waliofariki nchini Ufilipino jana (Alhamisi) baada ya dhoruba Phanfone kuzuka katika maeneo ya kati ya nchi hiyo imeongezeka hadi 21, serikali ya nchi hiyo imesema leo (Ijumaa).

Serikali nchini humo imesema takriban watu 10 bado hawajapatikana. Isitoshe, karibia watu 186,000 katika vijiji 584 waliathiriwa na dhoruba hiyo, na vilevile zaidi ya nyumba 2000 na shule 55 ziliharibiwa. Phanfone ni dhoruba ya ishirini na mojs kuzuka nchini Ufilipino huu mwaka

Comments