Je ni viumbe kutoka sayari ya mbali ndiyo waliyo jenga Pyramid? Part 2






Ndani    ya Pyramid kuna vyumba (vyemba) vilivyo jengwa juu, chini ya pyramid, kuna milango kama huo hapo kwenye picha ambao haujulikani unafunguliwaje na ndani ya chumba hicho kuna nini? Maduara meusi unayo ona ni matobo ambayo kamera imepenyezwa kuona kuna nini ndani. Walichoona ni mlango mwingne kama huo. Hakuna kibali kilichotolewa kuendelea kufanya utafiti kujua kuna nini ndani. Ni kipi tunacho ogopa?

Uwanda wa Gaza, nyumbani kwa Great Sphinx, na nyumbani kwa mapiramidi makubwa matatu ya Egypt, kwa kila hali ujenzi huo wakale ni fumbo kwenye sanaa ya ujenzi wa zama zetu, fumbo ambalo teknolojia yetu haijafikiriwa kulifumbua. Hii ni kwa sababu ni vichache sana vinavyo fahamika kuhusiana na mapiramidi hayo.

fig001.gif

Muonekano wa Great Pyramid

Mapiramidi hayo matatu makubwa yanahusishwa na makaburi ya mafirauni watatu, yaani Khufu, Khafre na Menkaure ingawa hakuna mwili wala alama yoyote ya ustaarabu wa Egypt wa zama hizo iliyo pata kupatikana ndani ya maumbo hayo ambayo kama ilivyo michoro na mapiramidi ya Nazca nayo mjengaji wake hajulikani ni nani.

download (1) (1).jpg

Khufu, Khafre na Menkaure
Katika Great Piramidi kuna alama ya mfalme Khufu ambayo inalenga kuashiria kuwa yeye ndiye mjenzi wa kazi ile au walau kazi ile ilifanyika katika zama zake, lakini utafiti unaonesha kuwa alama hiyo iliwekwa makusudi mwaka 1837 na mtu aliyeitwa Howard Vyse.

Jina la mfalme Khufu liliwekwa hapo kwa kughushi ili ionekane kanakwamba yeye ndiye muhusika wa ujenzi huo au ulifanyika katika zama zake.

Mengi yamesemwa kuhusu jamaa huyu kuamua kuipa nguvu ile nadharia ya kuwa Khufu ndiye mjenzi wa kazi ile kwa kuweka alama yake kwenye ukuta wa Great Pyramid. Hata hivyo lilokubwa ni kuwa Howard Vyese si wa kwanza kuingia ndani ya Pyramid na kutoa hadithi zake, na alama hizi za Khufu zimeonakana katika vyemba vinne vilivyo gunduliwa na Howard na alama hizo hakuzitaja popote katika maandishi yake mpaka siku ya pili alipokwenda na mtu mwingine katika vyemba hivyo.

Mwaka 1765 mtu aliyeitwa Davison alipogundua kuwepo kwa vyemba hivyo hakuona wala kutaja kwenye kazi zake jina la Khufu . Hivyo jina hilo lililenga kumpa mfalme sifa isiyo yake. Lakini katika mtirirko wa sura hii tutakuja kuona kuwa Piramidi zilikuwepo hata kabla ya kuja binaadam, lakini ni kazi ya nani hiyo ndiyo jukumu letu kwa sasa kumtafuta mjenzi wa kazi hizi za maajabu.
Baadhi a vyemba ndani ya Pyramid. Ustadi na maarifa yaliyo tumika kuvichonga vyemba hivyo, bado unavitia soni vyombo nza zana za kwenye zama zetu katika ujenzi na uchimbaji.
Uzito wa jengo hilo unakaribia kufikia tani milioni 6! Leo hii kwa teknolojia tuliyo nayo, na maendeleo katika fani ya ujenzi, mahesabu na elimu ya nyota bado itahitajika maajabu kusimamisha jengo mfano wa hili. Great Pyramid linafahamika kuwa ndiyo jengo kubwa, bora zaidi duniani na lililojengwa kwa mahesabu na vipimo yakinifu. Bado tunaendelea mpaka tupate majibu ya swali letu. Ila majukumu yanakuwa mengi nachelewa kupost next time ntajitahidi

Comments