Ili kuweka tumbo vizuri ni vyema kutumia mara kwa mara endapo tumbo linajaa gesi, au kukosa choo. Unachanga Baking powder na Vinegar kiasi, inapoanza kufuka kunywa.(Mfano wa dawa ya Andrews) Baada ya dakika kumi utaona tumbo lako lipo vizuri kabisa.
Kwa wale wanaotoa harufu mbaya mwilini, tumia baking powder kupaka kwenye kwapa au sehemu za siri.
Kwa wale wanaotoka vipele baada ya kunyoa ndevu, tumia baking power iwe kama after shave yako mara kwa mara!!!
Kwa wale wenye vipele vidogo vidogo (rashes). Tumia baking powder kwa kujisuuza baada ya kuoga. Kaa muda wa dakika 15. Jisuze kwa maji safi. Tumia kwa muda wa siku tatu. Vipele vyote vitakuwa vimekauka.
Tumia Baking Powder kidogo sana kuweka kwenye mboga za majani au njegele.Mboga itakuwa laini na rangi nzuri na kuvutia,
Nina hakika watu wengi mnatambua umuhimu wa Baking Powder kwa kupikia mandazi, mikate au keki.
Nina hakika watu wengi mnatambua umuhimu wa Baking Powder kwa kupikia mandazi, mikate au keki.
Wale wanaume wanaotoa harufu baada ya kuvua viatu, na vidole kuota fangasi, tumia Baking Powder kwa kuloweka miguu yako mara mbili kwa siku.
Ni matumaini kuwa watu wengi mtafurahia matumizi zaidi ya Baking Powder.
Note:Mwanamke usikose baking powder na vinegar jikoni kwako, kwa faida ya familia yako!!!!!
Comments
Post a Comment