KANSA YA SHINGO YA KIZAZI.




KANSA YA SHINGO YA KIZAZI.
Shingo ya kizazi(CERVIX) ni sehemu ya mfuko wa kizazi kuelekea kwenye njia ya uke.Sehemu hii ina kazi nyingi ikiwemo:1.Kupitisha mbegu za kiume kuelekea ktk mirijga ya uzazi ili kupevusha yai.2.Kupitisha damu ya hedhi.3.Ndio mlango anaopita mtoto wakati wa kuzaliwa kutoka ktk mfuko wa uzazi hatimaye ukeni.
Kama zilivyosehemu zingine za mwili,sehemu nayo inaweza kupata maradhi ikiwemo kansa.
Ugonjwa huu uwaathiri wanawake wengi wa rika zote waliokatika umri wa kuzaa.Miaka ya nyuma kabla ya maambukizi ya Ukimwi kugundulika Kansa ya Shingo ya Kizazi ilikuwa ikiwapata zaidi wanawake wenye umri wa miaka 45 na kuendelea.Lakini miaka ya hivi karibuni mwanamke yeyote aliye katika umri wa kuzaa anaweza kupata tatizo hili.
SABABU YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI.
Ugonjwa una sababishwa na virusi viitwavyo Human papiloma.Ambapo mtu anaweza kupatwa na hawa virusi wakati wa kujamiana na mtu mwenye maambukizi.
DALILI.
1.Kutokwa na majimaji au uchafu usio wa kawaida ukeni.
2.Kutokwa na damu ukeni hali ya kuwa siyo hedhi au umri wa kupata hedhi umekoma lakini anaona damu inatoka.
3.Kuhisi maumivu makali wakati wa kujamiiana.
4.Kutokwa na damu baada ya kujamiiana.
5.Kuwa na maumivu makali ya tumbo hasa chini kitovu au kwenye nyonga.
TABIA HATARISHI AU WALIOHATARINI
Je, ni tabia zipi hatarishi zinazoweza kupelekea kupata ugonjwa huu
1.Kuanza ngono mapema katika umri mdogo chini ya miaka 18
2.Uvutaji wa sigara
3.Kuwa na wapenzi wengi au kujamiiana na mtu mwenye wapenzi wengi
4.Matumizi ya mafuta mengi kwenye chakula au kula vyakula vyenye mafuta kwa wingi
5.Kutokula mboga za majani na matunda
6.Kuzaa mara kwa mara
7.Wenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
TIBA.
Kansa ya shingo ya kizazi inatibika iwapo itagundulika mapema ikiwa katika hatua za mwanzo.
Saratani ya shingo ya kizazi inapogundulika katika hatua za mwisho, uwezekano wa kutibika unakuwa ni mdogo na gharama za matibabu zinakuwa kubwa!
Utagunduaje mapema kama una saratani ya shingo ya kizazi?
Kufanya uchunguzi wa shingo ya kizazi angalau mara 1 kwa mwaka
KUMBUKA KANSA HII NDIYO KANSA INAYONGOZA KUSABABISHA VIFO NCHINI.

Comments