Kundi la vijana wasiokuwa na kazi hapo jana (Jumatano) waliandamana mbele ya bunge la Tunisia na kutishia kujiua kwa pamoja kulalamikia ukosefu wa ajira

Kundi la vijana wasiokuwa na kazi hapo jana (Jumatano) waliandamana mbele ya bunge la Tunisia na kutishia kujiua kwa pamoja kulalamikia ukosefu wa ajira
nchini humo, shirika la utangazaji la Tunis Afrique Presse (TAP) limeripoti.
Vijana hao ambao wote wamehitimu na shahada mbalimbali walijaribu kuingia kwenye jengo la bunge wakiwa wamejihami na mitungi ya gesi. Walihimiza spika wa bunge na manaibu wake kuwaahidi kazi vijana wa nchi hiyo kwa kutekeleza ahadi ya serikali ya kutoa ajira kwa vijana 183 wa mkoa wa Kasserine wanakotoka vijana hao. (Picha ya maktaba)

Comments