KUTOKWA NA DAMU UKENI (ABNORMAL UTERINE BLEEDING)
HILI
ni tatizo linalomtokea mwanamke aliye katika umri wa kuzaa, ni tatizo
ambalo husababisha damu itoke ndani ya kizazi kupitia ukeni.
Ni hali itokanayo na mabadiliko ya kawaida ya mifumo ya mwili. Hali hii inaweza kutokea katika mzunguko wa kawaida wa hedhi na wapo wanawake wengine huwatokea kwa kiasi kidogo wanapokuwa katika siku za upevushaji mayai.

Hali
ambayo siyo ya kawaida ya kutokwa damu ukeni ni pale damu ya hedhi
inapotoka nyingi na kwa muda mrefu au damu inaweza kutoka nyingi kwa
kufuata siku za hedhi na kwa muda wa zaidi ya siku saba au ikatoka
katika siku ambazo siyo za hedhi.
Mfano, umeshamaliza kubleed, unapumzika siku kadhaa halafu unaanza tena, hili pia ni tatizo kubwa na halihusiani na mzunguko wa hedhi.
Mfano, umeshamaliza kubleed, unapumzika siku kadhaa halafu unaanza tena, hili pia ni tatizo kubwa na halihusiani na mzunguko wa hedhi.
CHANZO CHA TATIZO NA UCHUNGUZI
Vipo vyanzo kadhaa vya tatizo hili ambavyo vinahitaji uchunguzi wa kina. Tutaanza kuvielezea kwa undani ili kama upo katika mojawapo ya makundi hayo uweze kuchukua hatua mapema.
Vipo vyanzo kadhaa vya tatizo hili ambavyo vinahitaji uchunguzi wa kina. Tutaanza kuvielezea kwa undani ili kama upo katika mojawapo ya makundi hayo uweze kuchukua hatua mapema.
Kwanza
ni tatizo la kutokwa na damu ukeni wakati wa ujauzito. Mwanamke
mjamzito hategemei awe anatokwa na damu ukeni, endapo itakuwa hivyo basi
chanzo kinaweza kuwa
kuharibika
kwa mimba, mimba kutungwa nje ya kizazi hasa kwenye mrija wa mayai,
damu kutoka katika kondo la nyuma, mabaki ya mimba iliyoharibika na
matatizo mengine ya kizazi ambayo kitaalamu wanawake wenye umri wa miaka
40 au ambao wana historia ya maambukizi sugu ya mdomo wa kizazi.
Tatizo
hili huonekana kwa kuchunguza mdomo wa kizazi. Hizi polyps au vinyama
ni vema vichunguzwe kwa umakini kwani wakati mwingine vinaweza kuwa ni
kansa. Uchunguzi wa kina utafanyika katika kliniki za madaktari bingwa
wa magonjwa ya kinamama.
Nne
ni kasoro za kizazi. Hapa kizazi kinaweza kuwa kimekaa vibaya au
hakijarudi vizuri baada ya kujifungua na ukajikuta damu inaendelea tu
kutoka kwa miezi kadhaa, kulika kwa mlango wa kizazi na kuvimba kwa
tabaka la ndani la kizazi, maambukizi sugu ya kizazi, vyote huchunguzwa
kitaalam na vipimo na utaratibu wa tiba utapangwa na daktari bingwa wa
akina mama.
Tatizo
la tano tunaita ‘endometriosis’. Hii ni hali ambayo tabaka la ndani la
kizazi linakuwa nje ya kizazi na humfanya mwanamke apatwe na mauvivu
makali ya chini ya tumbo na kiuno chote huku akiwa anatokwa na damu
kidogokidogo ukeni ingawa wakati mwingine huwa nyingi.
Hali hii husababisha ugumba, mwanamke hulalamika maumivu wakati wa tendo la ndoa na kuhisi uzito upande wa chini huku akipata shida wakati wa kukojoa na haja kubwa.
Hali hii husababisha ugumba, mwanamke hulalamika maumivu wakati wa tendo la ndoa na kuhisi uzito upande wa chini huku akipata shida wakati wa kukojoa na haja kubwa.
Tatizo
la sita ni magonjwa sugu mwilini mwa mwanamke kama tatizo la damu
kuganda, shinikizo la juu la damu, matatizo ya moyo, uwepo wa sumu
mwilini kutokana na mazingira ya kazi au unywaji wa pombe kupita kiasi,
magonjwa ya ini, ukosefu au upungufu wa vitamin B.
Kwa
ujumla uchunguzi hutegemea na historia ya ugonjwa na daktari
atakavyoona vinafaa. Tatizo hili pia linaweza kuwatokea watoto ambao
hawajavunja ungo, hivyo linapotokea ni vema uchunguzi wa kina ufanyike.
Saba
ni tatizo linalohusiana na mfumo wa homoni mwilini, hapa mgonjwa
atalalamika siku zake zinaenda bila ya mpangilio, hapati mimba na wala
hajui tarehe zake za kuingia kwenye hedhi.
Upevushaji
wa mayai haupo na hana historia ya kutumia njia ya kuzuia mimba kwa
madawa. Katika kundi hili pia mimba kwa kutumia sindano au vipandikizi
na sasa wanapata siku zao bila mpangilio.
Hawa tatizo kubwa linakuwa katika mfumo wa homoni au vichocheo na wanahitaji uchunguzi wa kina kwa madaktari bingwa wa matatizo ya uzazi katika hospitali za mikoa.
Hawa tatizo kubwa linakuwa katika mfumo wa homoni au vichocheo na wanahitaji uchunguzi wa kina kwa madaktari bingwa wa matatizo ya uzazi katika hospitali za mikoa.
NINI CHA KUFANYA?
Endapo unashabihiana na mojawapo ya makundi hapo juu, basi unashauriwa uwaone madaktari kwaharaka
Endapo unashabihiana na mojawapo ya makundi hapo juu, basi unashauriwa uwaone madaktari kwaharaka
Tumeona
baadhi ya sababu mbalimbali, basi usichelewe ili tatizo lisije kufikia
mahali ambapo gharama za kutibu zitakuwa kubwa, muda utakuwa mrefu au
lisitibike kabisa.
Comments
Post a Comment