Maafisa
waandamizi 21 wa Jeshi la nchi ya Bangladesh hivi karibuni wametembelea
Tanzania kujionea vivutio mbalimbali vya kitalii ikiwa ni pamoja na
Ngorongoro na Zanzibar.
Maafisa
hao, kutoka Chuo cha kijeshi kiitwacho Bangladesh Defence services
Command and Staff College cha mjini Dhaka walipata hamasa ya kutembelea
Tanzania baada ya mwanafunzi mwenzao na afisa wa JWTZ Meja Rajabu
Mangapi aliye mafunzoni chuoni hapo kufanya presentantion iliyohusu
utalii, viwanda, miundombinu na mikakati ya kuipeleka Tanzania katika
uchumi wa viwanda.
Presentantion
hiyo ilihudhuriwa pia na wafanyabiashara wakubwa ambao pia walihamasika
vilivyo na kuonesha nia kuja kuwekeza Tanzania kwa kujenga viwandani.
Watalii hao wamemwambia ripota wetu aliyeko Ngorongoro kwamba hawakuweza kuamini macho yao kuona wanyama wa aina zote wakiishi bega kwa bega na wanadamu huko 'Shimoni' Ngorongoro, na kuuliza endapo kama eneo hilo sipo ilipotua Safina ya Nuhu baada ya dhoruba?
Walimshukuru sana Meja Mangapi ambaye presentation yake ya kuvutia iliwafanya wafikie uamuzi wa kuja kujionea wenyewe, na kukuta kumbe walichooneshwa na mwanafunzi mwenzao huy pale chuoni kumbe ni theluthi tu ya maajabu ya Tanzania.

Maafisa kutoka Chuo cha kijeshi cha Bangladesh Defence services Command and Staff College wakitembelea Ngome Kongwe huko Zanzibar wakati wa kutalii Tanzania |
Maafisa kutoka Chuo cha kijeshi cha Bangladesh Defence services Command and Staff College wakitembelea Bwawa la Viboko huko Ngorongoro wakati wa ziara yao ya kitalii nchini Tanzania |
Maafisa kutoka Chuo cha kijeshi cha Bangladesh Defence services Command and Staff College wakijitayarisha kuingia 'shimoni' Ngorongoro wakati wa ziara yao ya kitalii nchini Tanzania |
Comments
Post a Comment