Madhara na tiba dhidi ya ugonjwa wa homa ya ini aina ya Hepatitis B



Homa ya Hepatitis B hutokana na kirusi kinachoambukizwa kupitia kwenye damu na majimaji mengine ya mwili, na ambacho huvamia ini na kusababisha vifo vya watu wapatao 650,000 kila mwaka, wengi wao wakiwa katika nchi za kipato cha chini na kipato cha wastani.
Shirika la Afya Duniani, WHO ambalo ni kinara katika makabailiano ya  magonjwa mathalani homa ya ini aina ya Hepatitis B hivi karibuni limetoa mwongozo wake wenye mapendekezo sita kuhusu matibabu ya ugonjwa huo.

Baadhi ya mapendekezo hayo ni jinsi ya kutafiti homa imeenea kwa kiasi gani, Kuamua nani anahitaji matibabu, Matibabu yapi yatumike awali na yapi yafuatie ikiwa ya awali hayakufanya kazi, na pia jinsi ya kufuatilia mambo manne ambayo ni kuangalia kama kuna saratani ya ini, na  kiasi gani ugonjwa wa ini unavyoendelea. Kuangalia kama matibabu yanafanya kazi na madhara yaletwayo na tiba hiyo.
Inakadiriwa kuwa watu milioni 240 kote duniani wana kirusi cha Hepatitis B, idadi kubwa ya maambukizi ikipatikana bara Afrika na Asia.
Kutaka kufahamu hali livyo na hatua za kukabilina na ugonjwa huo katika nchi za Afrika, tuungane na John Kibego kutoka Uganda.

Comments