Mbowe atua mkutano wa Bavicha usiku akitokea Mwanza


Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe leo Jumatatu Desemba 9, 2019 saa 2:15 usiku amewasili katika mkutano mkuu wa Baraza la Vijana la chama hicho (Bavicha) unaofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam akitokea mkoani Mwanza.
Mapema asubuhi leo, Mbowe alikuwa Mwanza katika sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika yaliyofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba.

Baada ya kuwasili, Mbowe alikwenda kupumzika katika moja ya vyumba vilivyopo karibu na ukumbi huo, ilipofika saa 3:30 usiku aliingia katika ukumbi. Leo wajumbe zaidi ya 300 wa baraza hilo watachagua viongozi wa Bavicha.
Aliingia ukumbini hapo akiambatana na wabunge wa chama hicho aliokuwa nao Mwanza.
Wabunge hao ni Godbless Lema (Arusha Mjini) na John Mnyika (Kibamba). Pia alikuwa ameambata na Meya wa Ubungo, Boniface Jacob.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji ndio alifungua mkutano huo wa uchaguzi leo asubuhi.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Dk Mashinji aliwaonya vijana hao kuacha kushambuliana, badala yake wajikite kupanga mikakati ya kuhakikisha Chadema kinashinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni anatarajia kutoa hotuba yake kwa wajumbe wa mkutano huo

Comments