Mkurugenzi vyuo vikuu Juvicuf Taiafa Mhe.Amina Ally anawatakia heri ya sikukuu ya Krismasi wakristo wote Duniani.
23 DIS, 2019.
Ndugu Wananchi wezangu, kwanza nachukua nafasi hii kumshukuru Allah (S.W) kwa kutujaalia uhai na uzima wa afya miongoni mwetu.
Tunajua sote kwamba kila ifikapo Tarehe 25 Disemba ya kila mwaka, Taifa na Dunia kwa ujumla hasa kwa Waumini wa Dini ya Kikristo wanasherehekea sikukuu ya Christmas.
Hivyo, napenda kuchukua fursa hii kwa niaba ya JUVICUF kuwatakia kila la kheri katika kusherehekea Sikukuu ya Christmas.
Aidha, niwaombe madereva wa vyombo vya moto kuzidisha umakini zaidi kwani watumiaji wa barabara na wasafiri watokao sehemu moja kwenda nyengine huongezeka maradufu zaidi katika vipindi cha Sikukuu.
Hata hivyo, niwakumbushe wananchi wezangu kuitunza amani na usalama wako binafsi kwa kufuata sheria na kutoa taarifa kwenye mamlaka husika, dhidi ya mtu/kikundi cha watu kinacho kuhatarishia amani na usalama wako.
Mwisho niwaombe ndugu zetu wa Jeshi la Polisi kuzidisha nguvu zaidi katika kipindi hichi ili kudhibiti vitendo vyote viovu kwa wananchi wetu.
Nimalizie kwa kuwatakia nyote maandalizi mema na sherehe njema ya sikukuu ya Christmas.
Ahsante.
Mkurugenzi wa Vyuo Vikuu Juvicuf - Taifa.
Comments
Post a Comment