Mmoja afariki na wengine 30 kulazwa kwa kula mzoga wa nyama ya Nguruwe

Mtoto mwenye umri wa miaka 7 Mareni Namsukuma amefariki na wengine 30 wote wakazi wa kijiji cha Utengule kata ya Mambwenkoswe wilayani Kalambo mkoani Rukwa wanaendelea
kupatiwa matibabu katika zahanati ya Kalembe baada ya  kula mzoga wa nyama ya Nguruwe.
Wakiongea wananchi kijijini hapo wamesema chanzo ni mwanakijiji mwenzao kuwauzia  nyama ya nguruwe ambae  alikuwa amekufa    bila kujua kilichomuua .
Mwenyekiti wa kijiji hicho Wigani Namsukuma amesema baada  ya  kupata taarifa hizo waliamua kutoa taarifa polisi na  kuwakimbiza  wagonjwa  katika zahanati  ya Kalambe .
Afisa mifugo wilayani humo Dkt. Enos Luvinga amekiri kutokea  tukio  hilo  na kuwasihi wananchi  kuacha  tabia ya  kula  nyama ya mifugo  iliokufa bila kujua kilichowaua.
Tukio  la  pili  kwa  wananchi  wa kata  hiyo kudhurika kutokana na kutumia kitoweo  cha wanyama  waliokufa bila kujua sababu za vifo vyao.

Comments