Watu
watatu wakiwamo watoto wawili wa familia moja wamekufa baada ya
kuangukiwa na ukuta wa nyumba wakiwa wamelala usiku huku mmoja akifa
maji baada ya kusombwa na maji wakati akitoka kusherekea sikukuu ya
krismasi kufatia mvua zinazoendelea kunyesha wilaya ya Serengeti mkoani
Mara.
Tukio hilo limetokea jana saa mbili usiku wakati mvua ikinyesha katika Kijiji cha Nyabirikira kata ya Isenye wilaya ya Serengeti mkoani hapa ambapo watoto hao walikuwa wamelala usingizi mzito ndipo maji yakatoba ukuta wa nyumba yakajaa ndani kisha ukuta wa nyumba hiyo ukawaangukia na kusababisha vifo vyao na mmoja kujeruhiwa huku Joshua Juma mkazi wa kijiji hicho akisombwa na maji wakati akijaribu kuvuka maji yaliyokuwa yamejaa barabarani kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha usiku huo akiwa na wenzake wawili wakitoka kusherekea sikukuu ya Krismas.
Wakati hayo yakitokea ITV ikiwa kijijini hapo ikashuhudia daraja la Isenye likikatika na kusababisha abiria kukwama kwa saa kadhaa na wananchi wanaotembea kwa mguu wakishindwa kuvuka huku barababara za kijiji hicho zikijaa maji na kusababisha adha kwa wananchi.
Hata hivyo mkuu wa wilaya ambaye pia amefika kijijini hapo na kutoa msaada wa chakula kwa familia zilizopoteza wapendwa wao akitoa tahadhari kwa wananchi kutokatiza ovyo kwenye maeneo yaliyojaa maji.

Comments
Post a Comment