Najiuliza Mie Mtupori mshamba kutoka Moro

Najiuliza Mie Mtupori

Mtu kutoka Shamba Moro kama alivyokasema 😁😁😁


Ni Kitu Gani Dunia ?

Dunia ni eneo flani hivi ambalo lipo na limewekwa na Muumba  mwenyewe Kwa utaratibu aliotaka Mwenyewe .

Wengine husema kua Dunia ni moja ya Sayari inayotumiwa na Viumbe hai na Viumbe mfu.


Mimi mtupori mshamba kutoka Moro , nasema Dunia sehemu ambayo wenye majumba ya kulala wanakosa usingizi Kwa maradhi na wenye usingizi hawana pakulala wanalala Mitaroni .

Dunia ni pale wenye njaa hawana Chakula na wenye Chakula hawana hamu ya kula au wamekatazwa kula wavipendavyo Kwa sababu ya Maradhi.

Dunia ni pale wenye makosa wapo huru na watu waso hatia wapo Magerezani Kwa kubambikiwa Kesi.

Dunia ni pale ambapo wengine tunatafuta watoto na wengine wanavitupa vichanga Mitaroni.

Dunia ni pale aso na Miguu anatamani apate Miguu wakati mwenye Miguu anatamani apate Baiskeli na mwenye Baiskeli anatamani apate Pikipiki , Mwenye Pikipiki anatamani apate Gari mwenye Gari anatamani Bombadia , hii ndio Dunia kifupi Dunia ni Maisha flani hivi yenye ubinafsi wa tofauti ya  Viwango.

Wewe unatamani uwe nani ? Uweje ? Uwe na nini katika hii Dunia ?

Alhamdulillah mie natamani niwe Kwa alivyonikadiria Mola wetu Mtukufu na sina kinyongo na Makadiru yake Allah.

Comments