Maafisa wote wa kike watalazimika kufumua nywele walizosukwa zisizoendana na sheria ya mavazi ya polisi kuanzia tarehe 1, 2020, kwa mujibu wa idara ya Polsi nchini Kenya.
"Kuna haja ya kutambua kwamba kwamba sare ya polisi ni ishara ya mamlaka na inastahili kupewa shehima yake. Kuanzia Januari 1, 2020, nywele za mitindo isiyokubalika hazitakubaliwa," Bwana Mbugua amethibitisha.
Maafisa wa kike wa polisi nchini Kenya watatakiwa kuondoa mitindo yao ya nywele pamoja na zile walizobandika katika kipindi hiki cha sikukuu.
Idara hiyo ya polisi inasema inataka kuhakikisha maafisa wote wanafuatilia kikamilifu mfumo wa mavazi rasmi ya kazi.
Aidha hatua hii inaenda sambamba na sare mpya za polisi zilizotolewa.
Kanuni ya ukiukaji wa sare za polisi
Taarifa iliyotolewa mapema wiki hii, inasema kwamba makamanda wote wa polisi wa eneo wamepewa jukumu la kuhakikisha kwamba sheria ya mavazi inafuatiliwa vilivyo.
Sare ya Polisi
Inspekta Jenerali Mbugua amedai kuwa mitindo ya nywele zilizosukwa inafanya iwe vigumu kwa maafisa hao kuvaa kofia zao wakiwa kazini.
Bwana Mbugua ameonyesha wasiwasi wake juu ya hijabu za rangi kwa Waislamu akikisitiza kwamba wanastahili kuvaa hijabu rasmi nyeusi ya kitambaa chembamba kulingana na sheria.
"Nimeshuhudia vazi la kuhifadhi kichwa kwa Waislamu lililobadilishwa kulinganisha na makubaliano ya awali yaani kutoka mtandio mweusi hadi ile yenye rangi," amesema.
Comments
Post a Comment