Nini Cha Kufanya Kuhusu Ukimwi


Nini cha kufanya


1)Kama umepima na ukakutwa na VVU

A. Huo si mwisho wa maisha yako. Utaweza kuishi maisha marefu kama utakubali hali na kujifunza kuishi kwa matumaini.

B.Unawajibu wa kuwakinga na kuwalinda wengine usiwaambukize.

C.Kula vizuri, fanya mazoezi na tibu maradhi yoyote haraka

D.Kama upo tayari weka wazi hali uliyonayo kwa wale uliokaribu nao. Hii ni mbinu moja wapo ya kupambana na virusi visitumalize.

2) Kama umepima na huna VVU

Jilinde, hiyo haimaanishi una kinga ya virusi

Comments