Pinera alitoa wito wa umoja na maridhiano sio tu kwa waandamanaji, bali pia miongoni mwa umoja wa chama chake tawala
Katika hotuba ya usiku wa kuamkia siku ya Krismasi,rais wa Chile Sebastian Pinera alitoa wito wa kukomeshwa kwa zaidi ya miezi mbili ya maandamano ya kupinga serikali na ushirikiano mkubwa wa kisiasa
.
Pinera alitoa wito wa umoja na maridhiano sio tu kwa waandamanaji, bali pia miongoni mwa umoja wa chama chake tawala, Chile Vamos, ambacho kimegawanyika kutokana tofauti za maoni juu ya jinsi ya kushughulikia machafuko ya kisiasa na kijamii.
"Nchi iliyogawanyika ... haina mustakabali mzuri. Nchi ya umoja ambayo inaheshimu tofauti zake lakini ina uwezo wa kujenga pamoja ni nchi ambayo ina mustakabali mzuri," alisema Pinera.
"Tuache nyuma hisia hizi zote za mgongano, mgawanyiko, na mikutano na
tutafute kinachotuunganisha, badala ya kutafuta kinachotutengaisha,"
Pinera aliongezea.
Comments
Post a Comment