POLISI NCHINI SCOTLAND IMEIDHINISHA HIJAB KUWA SARE RASMI KWA POLISI WA KIKE WAISLAMU



Miaka15 nyuma polisi wa Scotland walipendekeza uvaaji wa Hijabu kwa polisi wa kike Waislamu kama watapenda kuvaa hijab na kama watapata idhini kutoka kwa maafisa waandamizi.



 Polisi Scotland imetangaza kwamba hijab itakuwa sehemu ya sare yake rasmi kwani inakusudia kuunda kikosi chenye watu wa aina tofauti tofauti ili kukidhi haja na mahitaji ya jamii.

Msemaji wa Jeshi hilo alisema kuwa _"wanatarajia hatua hiyo itawavutia na kuwatia moyo wanawake kutoka jamii za Waislamu nchini Uingereza, ambao hapo awali hawakuona kuwa kazi ya polisi ni chaguo lao"_.

Kabla ya hapo, maafisa Waislamu wa kike wa polisi uko Uskoti waliruhusiwa kuvaa hijab, lakini kama tu itapitishwa na maafisa waandamizi.

 Polisi wa Metropolitan waliruhusu hijab kama sare ya (hiari) jeshi mnamo 2001 kama sehemu ya harakati za usawa kwenye ajira..

Soma Habari Hii Zaidi.
👇🏿 https://www.independent.co.uk/news/uk/home-news/police-scotland-hijab-official-uniform-muslim-women-islam-muslam-veil-a7207106.html

Comments