Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema kwamba nchi yake itazidi kushikilia msimamo wake

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema kwamba nchi yake itazidi kushikilia msimamo wake
dhabiti hadi pale Washington itakapolazimika kubadilisha sera zake dhidi ya Tehran.
“Wamarekani hawana namna isipokuwa kubadilisha mkondo wao. Tutawalazimisha kubadilisha sera zao kupitia ukinzani na uvumilivu,” Rouhani alisema hayo jana (Jumatano) akiwa nchini Malaysia. Rais huyo aliongeza kwamba vikwazo vya Marekani dhidi ya nchi yake havitadumu muda mrefu. Rouhani alisema kuwa nchi yake imebuni njia za kutumia ukinzani kubadilisha vikwazo hivyo ili viwe vya manufaa. (Picha ya maktaba)

Comments