Rais wa Zambia Edgar Lungu amewasamehe wafungwa 961 katika shamrashamra za Krismasi na Mwaka Mpya,


Rais wa Zambia Edgar Lungu amewasamehe wafungwa 961 katika shamrashamra za Krismasi na Mwaka Mpya, waziri wa mambo ya ndani nchini humo Stephen Kampyongo alisema jana (Jumanne).
Kwa mujibu wa Stephen, wafungwa hao walikuwa wakitumikia vifungo vya muda mfupi kati ya miezi mitano na sita, huku wafungwa watatu walihukumiwa kifungo cha maisha gerezani. Idadi wa wafungwa nchini humo kwa sasa ni 22, 823

Comments