Saikolojia Inavyotatua Tatizo La Mwanaume Kufika Kileleni Mapema

!


Malalamiko yanayotolewa na baadhi yao yanaonesha kwamba, muda wa kumaliza tendo huwa kati ya nusu dakika na dakika tatu kwa tendo la kwanza, huku wengine wakimaliza hamu katika hatua za awali tu za hamasa ya kimahaba.
Hata hivyo, kumetolewa maelezo na nafuu ya ongezeko la muda katika tendo la pili na kuendelea, ingawa bado suala la kutangulia kufika kileleni kabla ya wanawake limekuwa likiwahuzunisha wanaume wengi.
Ni ukweli usiopingika kuwa, mwanaume anapowahi kufika kileleni kabla ya mwenzake humsababishia kero mwanamke anayeshiriki naye tendo, kwani humwacha njia panda pasipokuwa na hitimisho la raha ya kujamiiana.
Hali hii inatokana na maumbile ya uume wa mwanaume ambao husinyaa mara baada ya kuhitimisha mbio zake, lakini kwa mwanamke kuwahi si tatizo, kwani hakumfanyi ashindwe kumsindikiza mwenzake hadi kileleni.
Utofauti huu ndiyo unaowafanya wanaume wahuzunike zaidi wanapokabiliwa na janga hilo kiasi cha kufikia hatua ya kwenda kwa waganga/matabibu ili iwasaidie kuepuka balaa ya kutoka uwanjani na aibu.
Ingawa kumekuwa na mafanikio katika tiba za kisayansi, lakini bado wanaume wameshindwa kupata ukombozi wa kudumu wa tatizo hili. Wengi wamejikuta wakijiongezea mzigo wa fikra kwa kuzitumaini zaidi dawa au kuzitumia na kupata matokeo mabaya zaidi ya kuishiwa nguvu kabisa.
Kwa kufahamu mikinzamo iliyopo kati ya akili na tiba ya nguvu za kiume na madhara yachipukiayo imebainika kuwa, mtu anaweza kujitibu tatizo hilo kwa kutumia kanuni za kisaikolojia na mafanikio yasiyo na madhara yakapatikana.
Wataalamu wa kisaikolojia wanatambua kuwa kanuni ya ufanyaji mapenzi iko zaidi kwenye ubongo kuliko mwilini.
Kinachotokea hadi mtu akapata msisimko wa kufanya mapenzi si mwitikio wa mwili, bali ni utambuzi wa akili juu ya kiwango cha mapenzi kilichopokelewa kwenye ubongo unaojihusisha na hisia.
Usikose kumalizia somo hili wiki ijayo kwenye gazeti hili uweze kutambua mbinu za kuweza kulimaliza tatizo hili kisaikolojia. Ushauri wa masuala ya kimaisha na matatizo yote yanayohuzunisha unatolewa, wasiliana nami!
Leo tutaendelea kutoka pale tulipoishia wiki iliyopita, kama ifuatavyo. Inaelezwa kuwa, akili ikishiba vigezo na kutuma taarifa zenye usahihi kwenye mwili viungo hupokea hisia na kuanza kusumbua. Kwa msingi huo kama tunataka kufika kileleni mapema au kuchelewa lazima tucheze zaidi na akili kuliko mwili.
Katika hali ya kawaida nguvu ya kupenda inayomwingia mtu huwa kubwa, lakini suala la kupunguza ukubwa wa hisia lazima lipewe kipaumbele. Jambo kubwa linalowasumbua wanaume wengi wenye tatizo la kufika kileleni mapema ni kuwa na PUPA ya kufanya mapenzi.
Wengi wao hupokea hisia zilizokuzwa na kwenda nazo katika ufanyaji wa tendo la ndoa. Saikolojia inaelekeza kuwa ili mwanaume achelewe kumaliza, lazima apunguze mhemko unaotokana na kuona, kuhisi na kupagawishwa na staili au chombezo toka kwa mwanamke.
Anachotakiwa kufanya ni kutumia zaidi ya dakika 20 kufanya maadalizi na mpenzi wake kabla ya kuanza tendo. Hii itasaidia kuufanya mhemko wake ushuke na kumuongezea muda wa kumaliza.
Aidha mbinu ya kuidanganya akili lazima itumike ili kuzima taarifa za juu za uzuri wa mwanamke, maumbile na raha ya starehe isipokelewe kwa nguvu kubwa mwilini. Hii ikiwa na maana kuwa kuna kipindi inabidi fikra za mwanume zisihamasike sana kwenye tendo badala yake iletwe mawazoni hali ya kawaida, si ile ya kuweweseka na kuhema hema hovyo. Yafuatayo ni maelekezo ya msingi ya kufanya, ili mtu asifike kileleni mapema:
Mume na mke wanapoingia katika uwanja wa mapenzi wakae kwanza kwa muda, huku wakiwa wamejiachia na mavazi mepesi. Pili wacheze michezo mingi kwa muda mrefu bila kuanza kazi yao. Wakiwa kwenye hamasa hizo wasiwe kimya bali wazungumze na kuulizana maswali ya kimahaba.
Baada ya hapo mbinu nyingine ya kuzuia mbegu za kiume zisitoke ni ile ya kujibana. Inashauriwa kuwa mwanaume akiona dalili za awali za kumaliza bila kujali ametumia muda gani anachotakiwa kufanya ni kukaza misuli ya miguu na kuzuia mbegu kwa mtindo atumiao kuzuia haja ndogo isitoke.
Kujibana huko kunatakiwa kuende sambamba na kuacha kucheza shoo'. Pacha na hilo mwanaume anatakiwa kuidanganya akili kwa kuilazimisha iwaze jambo jingine hasa la kuhuzunisha ili kuharibu taarifa za raha zilizotumwa mwilini zisiendelee kufanyiwa kazi na hatimaye kumaliza tendo haraka.
Zoezi hili linaweza kuwa gumu katika hatua za kwanza kutokana na kukosea muda sahihi wa kujizuia, lakini mhusika akiendelea kujizoeza atajikuta anaweza na kupata uwezo wa kufanya mapenzi hata kwa saa nzima, hivyo kuondokana na tatizo hilo bila tiba wala madhara. Kwa ufafanuzi zaidi wa tatizo hili na upungufu wa nguvu za kiume nunua kitabu cha Saikolojia na Maisha.
Uwanja wetu wa leo, utakuwa na kazi moja tu, kujadili tatizo la kuwahi kufika kileleni, kuchelewa kupata nguvu za kurudia tendo, chanzo na tiba yake. Dhumuni la kuandika mada hii limetokana na maoni ya wasomaji wengi.
Wasomaji hao ambao wengi ni wanaume, waliniomba niwaandikie hivyo ili kunusuru uhusiano wao. Wengine wapo kwenye ndoa, kwahiyo waliniambia kuwa ushauri wangu unaweza kuwa tiba timilifu kwao.
Hivyo basi, kutokana na kutambua umuhimu wao, ndiyo maana sijasita kushika kalamu na kuandika haya unayoyasoma.
Tatizo la kuwahi kufika kileleni, mara nyingi huendana na mambo mengine ambayo huchagiza wenzi wengi kusalitiana ama kutengana kabisa.
Wanawake wengi wanagombana na watu wao kwa sababu kama hizi, hawavutiwi kuwaona waume wao wakiwahi kufika kileleni, hivyo kushindwa kuwapa dozi inayotosheleza.
Wanasikitishwa na hali ya wenzi wao ya kukosa nguvu za kutosha wakati wa kufanya tendo la ndoa ama ugoigoi wa kuchelewa kurudiwa na nguvu za kufanya kweli.
Aidha, wanakosa amani wanapobaini kwamba wapenzi wao hawana msisimko wakati wa kufanya yale mambo yetu'. Hata hivyo, tunapogeuka kisaikolojia hili si tatizo kubwa, bali linahitaji kutuliza akili.
Ninaposema kutuliza akili, nakuwa namaanisha kuwa wengi hawana magonjwa yanayohitaji dawa, isipokuwa wanasumbuliwa na matatizo ya kisaikolojia tu.
Vijana na baadhi ya watu wazima wengine wanaenda kwa waganga na wakati mwingine wakijikuta wanajiingiza katika matumizi ya mitishamba bila kuelewa kwamba ugonjwa wao haupo kwenye kasoro za kimaumbile, bali upo akilini.
Hapa nataka tukubaliane kwamba jambo kubwa linalowasumbua wanaume wengi wanaodai kuwa hawana nguvu ni ukosefu wa elimu ya mabadiliko ya kibinadamu na ufahamu duni wa mbinu za kuwawezesha kucheza michezo ya kimapenzi kwa ufanisi.
Mpenzi ni sanaa pana, ina mafunzo mengi na ili uimudu, unatakiwa ujifunze kila siku mabadiliko yaliyopo. Sambamba na hilo, kujua mapito, mazingira, mabadiliko ya mwili na kuyakubali ni mambo ya msingi.
Pamoja na matatizo haya kuwakera wanawake kama nilivyotangulia kusema, huwafanya wanaume kukosa amani. Mara nyingi wanaopata dosari hizi, hujihisi wana nuksi.
Hata hivyo, mshangao unaokuja hapa ni kwamba wanaume hupenda kutafuta mbinu za kutatua tatizo lao bila kuwashirikisha wenzi wao, kana kwamba wao haliwahusu.
Saikolojia inatambua kuwa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume ni zao la udhaifu wa mke na mume na sio la mwanaume peke yake kama watu wengi wanavyodhani.
Kwa mfano, mwanaume atapata wapi msisimko wa kimahaba kama mwanamke hatakuwa mtundu wa kubuni mbinu za kuufanya mwili uliopoa usisimke?
Atavutiwa nini mwanaume kurudia awamu ya pili, ikiwa kwenye mzunguko wa kwanza alikutana na harufu isiyofaa? Nakshi nakshi humuongezea mwanaume hamu ya kutaka tena na tena. Huo ndiyo ukweli!
Napenda niweke ukweli kweupe, mara nyingi tatizo la msisimko wa kurudia tendo, husababishwa na mwanamke mwenyewe. Kwa maana hiyo, ili litatuliwe ni lazima ziwepo juhudi za pande mbili.
Tuweke kituo kwa leo, nakuomba tukutane Jumatatu ili tuendelee na mada hii. Bila shaka, tutakapokutana ishu' ijayo, utaweza kung'amua mengi kuhusu somo hili. Mimi na wewe tupo together as one

Comments