Saikolojia Na Uwezo Mkubwa Wa Kufikiri




Katikamaisha ya kila siku, kuna changamoto mbalimbali zinazotokana na jinsi binadamuanavyoingiliana baina yake na jamii inayomzunguka. Nimekuwa nikitafakari namnaya kukabiliana na changamoto hizi nikabaini kuwa “Saikolojia na uwezo mkubwa wa Kufikiri” ndiyo mihimili pekee inayowezakukabiliana na changamoto hizi. Ukiwa na misingi imara ya nguzo hizi, zitakuwezeshakung’amua na kutoa maamuzi sahihi katika changamoto mbalimbali zinazotokana namuingiliano wa mwanadamu na maisha yake kwa ujumla.
Lengola kuwashirikisha katika mada hii, ni kutaka kujua mbinu zinazowezakumtambulisha mwanadamu kama anaongea ‘Ukweli’au ‘Uongo’ kutokana na muonekanowake mnapokuwa mkiongea naye (Facial Expressions). Binafsi, nimeona Saikolojiana uwezo mkubwa wa kufikiri ndiyo nguzo muhimu katika intelijensia ya maisha yakila siku. Hivyo basi, nakaribisha majadiliano ili tuweze kuzifafanua kwa kinanguzo hizi pia tuongezee katika hizi nilizozitaja kwa lengo la kuboresha kwamanufaa ya wote.
Mimisi mwanasaikolojia na pia si mwanaintelijensia na niliyoyaandika hapa ni mawazoya kufikirika tu. Mawazo haya hayajanukuliwa kutoka chanzo chochote cha habarina yanaweza kuwa yamekosewa kwa namna moja au nyingine, basi yanaweza kurekebishwakwa kadri ya ufahamu wenu ili tuweze kupata mawazo sahihi yatakavyokubalika nawachangiaji wengine.
Saikolojianinayoizungumzia hapa, ni ile ya utambuzi wa mawazo ya binadamu kwa wakati huomnapokuwa mnawasiliana. Saikolojia hii ni ile inayowezesha kumtambua binadamukuwa anawaza nini kwa wakati huo mnapowasiliana. Hii inawezakuwa mavazi yake,jinsi anavyoongea, na muonekano wake kwa ujumla. Kwa mfano, kutambua kamaanadanganya au anasema ukweli kulingana na jambo mnalo zungumzia kwa wakati huoinaweza kudhihirishwa na aidha kuangalia pembeni, kupepesa kope mara nyingi,kutokuwianisha maongezi yake ya awali na maongezi anayoendelea kuongea, n.k.
Uwezowa kufikiri ninaouzungumzia katika mada hii, ni ule uwezo wa kufikiri nakutafakari jambo husika kwa mapana yake ambao humuwezesha muhusika kubaini aidhajambo hilo lina madhara au linajenga kulingana na hali iliyopo. Kwa mfano,“wewe unaishi Gongolamboto na kazi unafanyia Masaki, siku moja upo ofisinijirani yako ambaye huwa mnawasiliana naye kila siku unapokuwa nyumbani, amekujaofisini kwako anaomba msaada wa pesa, hujawahi kumtamkia ni kazi gani unafanya nani wapi unafanyia kazi”.
Hapani lazima “kwa nini?” zitakuwa nyingi! Maswali ya kujiuliza hapa ni kama vile,amejuaje kama nafanyia kazi Masaki? Nani kamuelekeza hapa ofisini kwangu? Je,mimi ndiyo ameona ninauwezo wa kumsaidia kiasi hicho cha pesa? Hivi ni kweliamekuja kuomba pesa au kuna jambo lingine nyuma ya pazia amekuja kulichunguza?n.k.
Wanasaikolojia na wengine wote wenye ufahamu na jambo hili mnakaribishwakwa mjadala

Comments