Panic attack ni nini?
Panic attack ni uoga mkubwa unaompata mtu.uko kwenye kundi la magonjwa ya wasiwasi (anxiety disoders). Uoga huu huweza mpata mtu kwa sababu maalum kama vile kuona nyoka. Pia inaweza kutokea bila hata sababu maalum, yaani unaweza ukawa umetulia tu na kushangaa unapata dalili zifuatazo.
Uoga, kutetemeka, moyo kwenda mbio, kutetemeka na kutoka jasho, maumivu ya kifua, kuhisi kushindwa kupumua, kuhisi kukabwa kooni, kuhisi kichefuchefu, tumbo kuchafuka , kuhisi kizunguzungu na kuzimia, kuhisi kuchanganyikiwa na kuhisi kufakufa, kutojitambua (kujihisi kama sio wewe).
Watu wengine hali hii huwapata usiku wakiwa usingizini. Watu hawa hushtuka na kuhisi walikuwa wanakabwa na wachawi au wamepata heart attack lakini ukweli ni kuwa wamepata panic attack. Hali hii kama inatokea mara kwa mara linaweza kumuathiri sana mtu akiwa kazini,shuleni na maisha yake kwa ujumla. hii nikwasababu mtu anaanza kuogopa kujumuika na watu kwa kuogopa hali hii kumkuta.
Watu 30 kati ya 100 hupata panic attack walau mara moja maishani. Pia watu 3 kati ya 100 tatizo hili hujirudia ruudia na tunasema wanapanic disorder. Pia inasemekana kati ya watu 100 wanaoenda kuwaona madaktari wa moyo 60 huwa ni panic attack. Wanawake wanauwezekano mara mbili wa kupata panic attack ukifananisha na wanaume.
Nini husababisha panic attack?
Hali hii husababishwa ubongo kuwa na uwezo mdogo wa kuhimili uoga. Pia kuna hali inaitwa anxiety ambayo mtu anakuwa na wasiwasi sana na maisha yake au afya yake. Hali hii inaweza kusababisha kupatwa na panic attack. Pia maisha ya stress huweza kumsababishia mtu kupata panic attack.
Matibabu
Matibabu
Matababu ya kwanza hulenga kumuondolea mtu wasiwasi (anxiety) na kumuondolea stress maishani.kuondoa wasiwasi hujumuisha mafunzo ya kurelax na kumuexpose mtu kwenye mazingira yanayomletea attack ili ayazoee. Pia kupata elimu kuhusu hali hii ni sehemu ya matibabu. Pia kuna mbinu mbali mbali za kupunguza stress.
pia Kuna dawa za kutibu kama alprazolam ambayo hutumika kwa matibabu ya muda mfupi na dawa kama clomipramine kwa matibabu ya muda mrefu.
Kwa msaada wa kitabu abnormal psychology cha Robin Rosenberg na Stephen Kosslyn.
wenu katika kupani Red Giant
wenu katika kupani Red Giant
Kwa kawaidamtu akikutana na kitu anakiogopa hali zifuatazo humpata.
1.Moyo huenda mbio ili kupelaka sukari na oksijeni kwa wingi kwenye misuli na ubongo kujiandaa kupambana au kukimbia.
2.Jasho kidogo hutoka mikononi kumuwezesha kukamata vitu vizuri.
3.Damu inapungua kwenda maeneo yasiyo muhimu kama kwenye ngozi na tumboni na kunakuwa na hali ya kutaka 4.kutapika,kujisaidia au kukojoa. Ndiyo maana wengine hujisaidia wakiogopa.
5.Ngozi hupauka sababu damu nyingi huenda kwwenye misuli na ubongo.
6.Pia mwili hukakamaa, pengine ndiyo husababisha kutetemeka.
Haya ni mambo ya kawaida mtu aogopapo ila yakizidi au yakiwa makubwa ndiyo tunaita panic attack/disorder. Hii inaweza pelekea mtu kuogopa kufanya baadhi ya vitu kama presentation. Lakini pia mtu anaweza kuwa anaogopa kufanya presentation sababu ya socialphobia/agarophobia ambazo tutazungumzia siku nyingine.
Njia nzuri ni kunywa dawa ya propanolo kidonge nusu saa kabla ya presentation. Hii dawa mara nyingi hutibu moyo hivyo ni vizuri ukamuona mtaalamu wa dawa au ukatafiti
Comments
Post a Comment