Serikali ya Rwanda imewahamisha takriban raia 6,000 kutoka maeneo yaliyotishiwa na mvua nzito

Serikali ya Rwanda ilisema jana (Jumatano) kuwa imewahamisha takriban raia 6,000 kutoka maeneo yaliyotishiwa na mvua nzito katika kipindi cha wiki tatu za kwanza za mwezi wa Disemba, waziri wa serikali nchini humo Anastase Shyaka alisema.
Kwa mujibu wa Anastase, takriban raia 4,000 walihamia kwa jamaa zao, 1,500 walihamia katika nyumba zilizokodishwa na serikali, na vilevile wengine 300 walihamia mashuleni kwa muda mfupi.
Kulingana na takwimu za ujumbe ya ofisi ya shirika la kimataifa linalohusika na uratibu wa masuala ya kibinadamu (OCHA), watu wapatao 280 walipoteza maisha yao na zaidi ya watu milioni 2.8 waliathirika kutokana na mvua nzito na mafuriko kufikia mapema Disemba mwaka huu.

Comments