Tatizo la harufu mbaya ukeni ( bad vaginal smell)
Leo
tutazungumzia tatizo linalowasumbua wanawake wengi, tatizo la kutokwa
na uchafu unaotoa harufu mbaya sehemu za siri. Kitaalamu hali ya
mwanamke kutokwa na majimaji yenye rangi nyeupe au ya njano,ni hali ya
kawaida na wala siyo tatizo
endapo majimaji hayo siyo mazito sana na wala hayatoi harufu mbaya. Lakini endapo majimaji yanayotoka yapo katika hali ya ute
mzito wenye rangi nyeupe au kahawia, yanatoa harufu kali na yanawasha, basi hiyo ni ishara ya ugonjwa uitwao Vaginosis.

Majimaji
au ute unaoteleza kutoka sehemu za siri ni njia inayowezesha viungo vya
uzazi vya mwanamke kujisafisha na kuutoa uchafu wa seli zilizokufa na
mabaki ya damu ya hedhi nje ya mwili. Pia huvikinga viungo vya uzazi
dhidi ya maambukizi ya
bacteria au fangasi wanaoleta magonjwa. Kwa kawaida huwa hayatoi harufu na huwa na rangi nyeupe au ya njano. Pia
huwa na asidi ya Lactic ambayo huzuia kuzaliana kwa vijidudu vya maradhi na huzalishwa kwenye tezi za Bartholin (Bartholin's glands) zilizopo kwenye shingo ya mlango wa uzazi (Cervix).

Kwa
kawaida, mwanamke hutoa kiasi cha gramu 2 za seli zilizokufa kutoka
kwenye mji a uzazi na gramu 3 za ute mwepesi kila siku. Kiwango hiki
huweza kuongezeka au kupungua kutegemeana na mzunguko wa hedhi. Kuna
wakati ute huwa mwepesi na unaovutika (kama ute wa yai la kuku) na kuna
wakati huwa mzito kiasi na wenye rangi ya njano. Ute huu ni wa kawaida
na huwatoka wanawake wote hususan baada ya kuvunja ungo.
Sababu za kutokwa na uchafu huo Kuna sababu nyingi ambazo husababisha mwanamke kutoa ute au majimaji yasiyo ya
kawaida kutoka kwenye sehemu zake za siri. Maambukizi ya bacteria wanaosababisha magonjwa kama Trichomoniasis, Candidiasis, Gonorhear au uambukizo wa bacteria Candida albicans, Vaginosis Bacteria n.k husababisha mwanamke kutokwa na uchafu unaoambatana na harufu mbaya.

Pia mabaki ya vitambaa, tissue au pedi ambazo hazikutolewa wakati wa hedhi huweza kusababisha tatizo hili. Usafi wa
sehemu za siri usipozingatiwa hususani mwanamke anapokuwa kwenye siku zake za hedhi, huweza kuwa mazalia mazuri ya
bacteria wanaosababisha harufu mbaya.

Dalili za ugonjwa wa kutoa harufu
Wanawake wenye tatizo la Vaginosis huwa na dalili kubwa ya kutokwa na ute na majimaji yasiyo ya kawaida (Uchafu) kutoka sehemu za siri. Uchafu huu huwa unatoa harufu kali kama shombo ya samaki au kitu kilichooza na huambatana na maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu.Wakati mwingine uchafu
wenye rangi kama ya kijani hutoka

-Kuwashwa na kuchomachoma sehemu za siri, mgonjwa asipopatiwa tiba haraka husababisha vidonda sehemu za siri.
- Mwanamke anapoona anatokwa na ute uliochanganyikana na damu hata kama hayupo kwenye siku zake, hii ni dalili nyingine
ya Vaginosis.
- Maumivu makali wakati wa tendo pia ni dalili za ugonjwa
huu.
Matibabu
Tatizo hili hutibika hospitalini baada ya vipimo vya kitaalamu kuchukuliwa na daktari au nesi mwenye uzoefu wa kutosha
juu ya magonjwa ya wanawake. Dawa za kupaka (Ointment/ Cream) na dawa za kumeza (Pills) huweza kumaliza tatizo hili.

Angalizo:
Dawa za kihospitali muda mwingine zinaweza kukuongezea tatizo badala ya kukutibu, hivyo basi inashauliwa kuzingatia usafi wa nguo za ndani na ukeni kwa ujumla vilevile kuzingatia ulaji wa lishe bora ambayo itakusaidia kuuwezesha mwili kujisafisha wenyewe. Bila kusahau unywaji wa maji kwa wingi.

Kumbuka: Ni makosa kutumia dawa bila kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari au nesi.
Jihadhari
wanawake wengi hupenda kutumia baadhi ya dawa ukeni kwa lengo la kuongeza vionjo kwenye mapenzi pia kuufanya uke
kunukia vizuri vitu hivyo ni kama sabuni za kukaza uke, shabo inayowekwa kwenye maji machafu ili kusafisha wenyewe
huweka ukeni ili kukaza uke, dawa za kusafishia ukeni hasa zenye kemikali, hudi asali na vingine vingi naomba niseme kuwa
njia hizi hufurahisha kwa mda mfupi lakini madhara yake ni makubwa kama hivyo kuanza kutoa harufu mbaya.

Comments
Post a Comment