Tofauti kati ya Mahusiano na Ndoa




Tofauti kati ya Mahusiano na Ndoa.

Katika darasa la Saikolojia, mwanafunzi alimuuliza professor nini maana ya mahusiano ya kimapenzi? Professor akasema "ili niweze kukujibu swali lako nenda kwenye shamba kubwa la ngano na uchague mche wa ngano ulio mkubwa kuliko miche yote katika hilo shamba.

Kisha urudi nao hapa kipindi kitakachokuja. Ila sheria ni kwamba unapotafuta huo mche mkubwa kuliko yote katika hilo shamba huruhusiwi kurudi nyuma kutizama tena.

Mwanafunzi wa Saikolojia akaenda shambani na kuanza kutafuta mche mkubwa kuliko yote, alipopita tuta la kwanza aliona mche mkubwa lakini akajisemea kwamba niende tuta la pili labda huko kuna mkubwa zaidi, akenda tuta la pili nako akaona mche mkubwa, lakini akajisemesha vile vile kwamba huenda kuna mkubwa zaidi tuta la tatu, akendelea mpaka akaona kwamba matuta mengine yote yanayofuata yana miche midogo zaidi bora ya matuta ya nyuma.

Akajilaumu kukosa mche wa ngano katika matuta ya nyuma na hivyo akarudi darasani kwa Professor mikono mitupu. Professor akamwambia "hiyo ndio maana ya mahusiano, unakazana kutafuta yule aliye bora na amekamilika, lakini baadae unakuja kutambua kuwa ulipoteza mtu bora zaidi katika huo mchakato wako."

"Kwaio ndoa ni nini?" Mwanafunzi akamuuliza tena professor. Mwalimu akamwambia "ili niweze kukujibu swali lako, nenda katika shamba la mahindi na uchague mmea wa mahindi mkubwa kuliko yote katika shamba na urudi hapa, ila sheria ni ile ile huruhusiwi kurudi nyuma kuchukua yale uliyoyapitia"

Mwanafunzi akaenda katika shamba la mahindi, ila safari hii alikuwa muangalifu kutokurudia kosa la mwanzo, alipofika katikati ya shamba akachagua mmea wa mahindi ambao upo saizi ya kati ambao aliona unaridhisha na akarudi nao kwa mwalimu.

Professor alipomuona akamwambia, "safari hii umeleta mmea wa mahindi, umechukua ule ambao umeona unafaa, na umeamini kwamba huu ndio mzuri na umeizidi miche yote, "Hii ndio maana ya ndoa"

Comments