Uganda imechukua taji la mashindano ya Cecafa baada ya kuchapa Kenya 2-0 katika fainali katika mashindano hayo upande wa kina dada chini ya umri wa miaka 17.

Katika mechi hiyo iliyochezwa katika mkoa wa kati wa Uganda wa Buikwe, Uganda ilifunga bao kupitia kwa Fuazia Najemba na Juliet Nalukenge.
Ushindi huo umefanya Uganda kuibuka na alama 13 na kuwa mabingwa wa mashindano hayo ambayo yalichezwa kwa msingi wa robin.
"Tulifanya kazi kama timu na tukashinda michezo minne na kutoka sare
moja. Tumefurahi kuinua kombe hili," alisema Najjemba baada ya mchezo.
Tanzania ilichukua nafasi ya pili katika mashindano hayo ikiwa na alama 11 na Kenya ya tatu ikiwa na alama saba.
Uganda, Tanzania, Kenya, Djibouti, Burundi na Eritrea zilishiriki katika mashindano hayo.

Comments
Post a Comment