Ukweli Kuhusu Ukimwi / VVU


Ukweli Kuhusu Ukimwi / VVU

  • VVU ni virusi vinavyosababisha Ukimwi. Mtu aliyeambukizwa ukimwi anaweza kuishi kwa miaka mingi akiwa na afya nzuri kabla ya kuonyesha dalili za ukimwi.
  • Kupima damu ndiyo njia pekee ya kubaini iwapo mtu ana VVU; huwezi kujua kwa kumtazama.
  •  Hakuna tiba ya VVU. Vikiingia mwilini mwako itaendelea kukaa humo na utaweza kuvisambaza kwa mwingine.
  •  VVU haviwezi kuenea kwa kukumbatiana, kushikana mikono, kuchangia sahani au kukaa pamoja na mtu mwenye VVU.
  • VVU vinaweza kuambukiwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa mwingiliano wa damu au majimaji ya ukeni au uumeni wakati wa 
1)Mapenzi yasiyo salama
2)Kuchangia vitu vyenye ncha kali kama wembe au sindano nk.
3)Kuongezewa damu.
4)Kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito.

  • Mtu yeyote anaweza kupata VVU kama hajajilinda. Watu wengi hawafahamu kama wameambukizwa kwani hawajapima.

Comments