SAA CHACHE KABLA YA HARUSI, HUU NDIO ULIKUA USIA WA BABA KWA BINTI YAKE ANAEOLEWA.
1.Mwanangu unakwenda kuolewa na Mwanaume (Mume) na siyo marafiki, Hakikisha haushindi kwa Marafiki sasa kama ilivyokuwa kabla ya kuolewa kwako,Umesikia Mwanangu.....Heshimu ndoa yako
2.Mwanangu SIRI ZAKO NA MUMEO ni MARUFUKU kuzitoa nje,Usifikiri kila unayemuelezea SIRI Zako na Mumeo anafurahia WENGINE wanakucheka,JIFUNZE KUTUNZA SIRI ZAKO NA MUMEO..Mwanangu
3.Mwanangu Wewe ni Mlinzi wa MUMEO...Mlinde kwa MAOMBI Kila WAKATI Usifikiri MAOMBI YAMEISHA ULIPOINGIA KWENYE NDOA,HAPANA UKIZUBAA TU,YULE MWIZI ATAKUJA
4.Mwanangu Mimi na Mama Yako tumezeeka na mda wetu umetutupa mkono ila furaha yetu inaenda kutimia kwa kukulea, ukakua katika maadili na ndoa yetu sasa na wewe unaenda kupata yako tumetimiza ndoto yetu ya kukuona ukiwa mama ambaye atayaenzi yote mema na kuwa na ndoa itakayodumu kama yetu ikitawaliwa na furaha na upendo... Linda sana ndoa yako
5. Mwanangu ulipokua mdogo shuleni na nyumbani tulikusifu sana kuwa umechangamka na wajua kuongea kweli kweli tena umerithi kutoka kwa bibi yako ila mwanangu mdomo ule umezibwa rasmi leo yakupasa kuwa na maneno machache au ukimya kabisa maana katika ndoa uongeaji saaaaana ni kero kubwa .... Cha msingi msikilize mmeo.
6. Mwanangu leo unaolewa na mmeo mtakayeishi pamoja milele sio mwanasiasa au mshindani wa debate shuleni tafadhali epuka argument au mabishano yasiyo na msingi ili kujenga familia yenye furaha muda wote... mabishano ni sumu katika ndoa.
7. Mwanangu unaolewa, kule unakoenda kuishi tambua sio kituo cha redio au television bali ni nyumbani kwako wewe na familia yako hivyo ni marufuku kupokea au kusambaza habari za ndani na nje... Epuka umbea ni uchafu katika ndoa.
8. Mwanangu siku ulipojisikia kuumwa au shida yeyote mtu wa kwanza kumshirikisha alikua mama yako kisha baadae mimi, hakika ulifanya vyema kabisa ila sasa mwanangu kuanzia leo ikitokea jambo lolote mtu wa kwanza kumshirikisha awe mme wako.... muamini mmeo.
9. Mwanangu tumekufunza yote ila hatujakufunza mafunzo ya kivita na uasi tafadhali tambua kule unakoenda kuishi mmeo ana wazazi na ndugu zake, waheshimu kama ulivyokua unatuheshimu dumisha upendo tambua wao sasa ndio familia yako mpya.... Epuka kuwa mchochezi na chanzo cha migogoro na chuki NDOA ISIJEKUKUSHINDA.
10. Mwanangu siku zote amini chochote apatacho mtu ni majaliwa ya MUNGU usitamani maisha ya wengine, mvumilie mmeo kwa chochote alichonacho au apatacho, ridhika nae, mkumbatie mtie moyo muombee hakika mtafanikiwa ardhini na mbinguni maana MUNGU hujibu maombi yao wamtafutao kwa bidii wakizishika amri zake na kujituma katika kufanya kazi.. Epuka tamaa ya utajiri na mali nyingi.
Funzo:
Ndoa sio kitchen party au send off bali ni mfumo mpya wa maisha unaohitaji wawili wenye kutoka familia tofauti kuunda familia moja itakayounganisha na kuyaenzi yale yote mema ya pande zote na kuwa bora zaidi itakayodumu kwa mafanikio na amani pia furaha tele.
Comments
Post a Comment